Thursday, November 22, 2012

MTOTO WA SIKU NANE AFARIKI KWA KUNG'ATWA NA MBWA...

Mtoto mdogo wa kiume amekufa kwa huzuni baada ya kung'atwa mara moja na mbwa wa familia yao anayeitwa Jack Russell.
Mtoto huyo wa siku nane, Harry Bell alikufa kutokana na majeraha baada ya mbwa huyo kumshambulia wakati akiishi kwenye nyumba ya babu yake.
Polisi na wafanyakazi wa gari la wagonjwa walikimbilia nyumbani hapo Barabara ya Woodside, huko Ketley, Telford, mjini Shropshire, muda mfupi baada ya Saa 2 asubuhi ya Jumanne.
Lakini licha ya juhudi kubwa za madaktari kuokoa maisha ya mtoto huyo, alifariki katika Hospitali ya Princes Royal huko Telford.
Mama wa Harry, Mikayla mwenye miaka 19, alikuwa akiishi na wazazi wake, Gordon Bell mwenye miaka 42 na Teresa mwenye miaka 40, wakati shambulio hilo lilipotokea.
Polisi waliweka ulinzi mkali jana nje ya nyumba ya babu huyo yenye thamani ya Pauni za Uingereza 119,000 yenye vyumba vitatu vya kulala.
Mwanamitindo Mikayla, alijifungua mtoto huyo Novemba 12 na kusambaza picha za mtoto wake huyo katika ukurasa wake wa mtandao wa Twitter.
Alituma picha za mtoto wake huyo wa kiume akiwa kavalia nadhifu na aliandika: "Mwanangu Harry 12-11-12."
Katika hali ya kutia uchungu, siku moja tu kabla ya mtoto wake kuuawa, Mikayla aliyejisikia fahari: "Hakuna za kumdanganya mtoto huyu mdogo kukimbia mabusu mengi."
Msemaji wa Polisi alisema maofisa walikuwa wakisubiri majibu ya uchunguzi wa mwili wa mtoto huyo, na wameanza uchunguzi kujua mazingira yanayoweza kuwa yalisababisha kifo chake.
Dalili za mwanzo hatahivyo, zinaonesha kwamba mtoto huyo alikufa kutokana na kung'atwa na mbwa, alisema polisi.
Msemaji huyo alisema: "Polisi na gari la wagonjwa waliitwa nyumbani hapo kwa anuani ya Barabara ya Woodside, Ketley,  kuhusu mtoto huyo ambaye hali yake haikuwa nzuri.
"Alipelekwa katika Hospitali ya Princess Royal iliyoko Telford na madakatari lakini akafariki muda mfupi baadaye.
"Kama ilivyo kwa matukio yote ya vifo vya watoto wadogo, Polisi wa West Mercia wameanzisha uchunguzi kuweza kujua sababu hasa za kifo hicho."
Inafahamika kwamba mbwa aliyehusika katika tukio hilo, anadhaniwa kuwa ni mbwa mdogo wa familia hiyo na si mbwa hatari.
Mpelelezi Mkuu Inspekta Neil Jamieson alisema: "Uchunguzi wetu unaendelea lakini inaonekana kwamba mtoto huyo alikufa kufuatia kung'atwa na mbwa.
"Mbwa huyo Jack Russell, alikuwa akifugwa na familia yake na kwamba mnyama huyo kwa sasa amefungiwa.
"Uchunguzi wa mwili wa mtoto huyo utafanyika kujua sababu hasa za kifo chake lakini mpaka hatua hii haionekani kuwa ni tukio la kutisha.
"Familia iliyohusika wamehuzunishwa na kumpoteza mtoto wao. Hawakusudii kuzungumza katika vyombo vya habari kwa muda huu wa sasa na hivyo ningeomba mheshimu hilo na kuwapa nafasi kama familia kulishughulikia.
"Tunaungana na familia ya mtoto huyo katika wakati huu wa huzuni kubwa."
Maofisa wa Polisi walionekana jana kwenye nyumba hiyo, ambayo familia inaaminika kuishi kwa miaka mingi iliyopita.

No comments: