Kesi ya mama anayeshitakiwa kwa kumuua mtoto wake mlemavu na kumtupa katika choo cha shule, Redience Charles (31), imepigwa kalenda mpaka Novemba 21, mwaka huu itakapotajwa tena.
Mshitakiwa huyo ambaye ni mkazi wa Hombolo Bwawani, Manispaa ya Dodoma, alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Machi 29, mwaka huu akikabiliwa na mashitaka ya mauaji ya mtoto huyo aliyekuwa na miaka mitano.
Kesi hiyo iko mbele ya Hakimu Mkazi Adrian Kilimi wa Mahakama ya Wilaya ya Dodoma Mjini.
Hakimu Kilimi alisema kuwa kesi hiyo ambayo upelelezi wake haujakamilika, imepangwa kutajwa tena Novemba 21, mwaka huu na mshtakiwa ataendelea kukaa rumande kutokana na mashitaka hayo kutokuwa na dhamana.
Awali, ilidaiwa na Wakili wa Serikali, Lina Magoma kuwa Machi 7, mwaka huu, huko Hombolo Bwawani mshitakiwa alimuua Karim Salum.
Mtoto huyo aliyeuawa alikuwa mlemavu wa viungo na bubu ambapo mwili wake uligundulika kwenye shimo la choo cha Shule ya Msingi Hombolo Bwawani A ukiwa umeharibika vibaya.
Mtoto huyo enzi za uhai wake alikuwa akiishi na mama yake mzazi na baba yake wa kambo Benjamini Chipanha ambapo mshitakiwa huyo kabla ya kukamatwa, inadaiwa alikuwa akieleza kijijini hapo kuwa mtoto wake alikuwa amechukuliwa na wafadhili kwenda kulelewa mkoani Tanga.
Taarifa za awali zilimkariri Diwani wa Hombolo Bwawani, Mussa Kawea akidai kuwa, mshitakiwa licha ya kudai mwanawe amepata mfadhili wa kumlea mkoani Tanga, alijua kuwa mtoto hakuwa kwa mfadhili yeyote.
Kawea alisema kuwa Machi 7, mwaka huu walipata taarifa za kupotea kwa mtoto huyo baada ya bibi yake mzaa mama, Esther Kuyowona kutoa taarifa ya kutoweka kwa mjukuu wake.
Alisema licha ya mama kudai mwanaye yupo Tanga, wananchi walifanya msako na katika pitapita yao walisikia harufu katika choo cha shule na kutoa taarifa tena Polisi ambapo baada ya choo kuvunjwa kulikutwa mabaki ya mwili wa mtoto huyo ukiwa umeharibika vibaya.

No comments:
Post a Comment