![]() |
| KUSHOTO: Gereza hilo lenye ulinzi hafifu. KULIA: Lee Chapman. |
Wafungwa katika gereza lenye ulinzi hafifu wanaruhusiwa kutembelewa na marafiki wa kike na mara kwa mara wamekuwa wakimiliki dawa za kulevya na simu za mkononi, imedaiwa.
Madai hayo yasiyo ya kawaida yametolewa na Lee Chapman mwenye miaka 34, ambaye alitoroka kutoka gereza la Hollesley Bay, karibu na Woodbridge, huko Suffolk, ambako alikuwa akitumikia kifungo kwa makosa ya uchomaji mali kwa makusudi na ujambazi.
Chapman alitoroka kutoka jela na kupora nyumba sita ndani ya siku 11. Aliongezewa miaka miwili zaidi katika hukumu yake.
Mfungwa huyo kwa hivi karibuni alihamishiwa katika gereza lenye ulinzi hafifu, kabla ya kutoroka na kisha kukutwa na polisi akiwa amejilaza kwenye kichochoro mjini Peterborough na kushitakiwa kwa utoro.
Wakili wa Chapman aliieleza Mahakama ya Ipswich kwamba mfungwa huyo alijikuta kwenye wakati mgumu katika gereza hilo lenye ulinzi hafifu.
Oktoba 8 mfungwa huyo aliondoka chumbani mwake kupitia bomba la kutolea maji machafu na kudandia basi kutoka kwenye viwanja vya gereza hilo.
Wakati akiwa njiani kurudi Cambridgeshire, Chapman alivamia na kupora nyumba sita huko Bury St Edmunds, mjini Suffolk, katika siku 11.
Chapman aliiba vyakula pamoja na mashine za michezo ya Nintendo kutoka katika nyumba moja.
Mmoja wa wamiliki wa nyumba hizo alimkuta Chapman ndani ya nyumba yake akila chokoleti kutoka kwenye jokofu lake.
Mwanamke huyo alipomkabili Chapman, aliomba radhi, akarejesha funguo za nyumba alizozikuta humo na kisha kutokomea kusikojulikana.
Chapman baadaye alikutwa na polisi akiwa amelala mjini Peterborough mnamo Oktoba 9.
Aliieleza mahakama hiyo alikiri kutoroka kutoka jela na kufanya ujambazi.
Jaji David Goodin alimfunga jumla ambapo sasa miaka miwili itaongezwa kwenye hukumu yake ya awali.
Baada ya kesi Msemaji wa Magereza alikanusha kwamba kulikuwa na dawa za kulevya, simu za mikononi na wanawake kwenye Gereza la Hollesley Bay.
Alisema: "Ni kosa la jinai kumiliki dawa za kulevya au simu ya mkononi katika gereza na mfungwa yeyote anayekutwa akimiliki vitu hivyo anakabidhiwa kwa polisi.
"Tunalichukulia suala hili kwa umakini mkubwa mno na wafanyakazi wanashughulika kutoa kila kitu kilichokatazwa gerezani, wakishirikiana na mamlaka husika pamoja na polisi.
Kuhusu madai ya Chapman kwamba wanawake wamekuwa wakilala kwenye gereza hilo, alisisitiza: "Madai haya haya si ya kweli hata kidogo."

No comments:
Post a Comment