| Mshiriki wa Epiq Bongo Star Search (EBSS) 2012, Walter Chilambo kutoka Dar es Salaam akiwa ameshika mkoba wenye fedha taslim Shilingi milioni 50 alizozawadiwa kwa kuibuka mshindi wa shindano hilo na kuwabwaga wenzake wanne (Nshoma, Nsami, Wababa, Salma) katika kinyang'anyiro kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo. Dalili za Walter kuzoa mamilioni hayo zilianza kuonekana mapema kwa jinsi alivyokuwa makini kwenye kuchagua na kuimba nyimbo mbalimbali. Baada ya kubaki washiriki wawili, ilijulikana bayana mshindi hasa kwa kuzingatia kuvurunda kwa mpinzani wake mshiriki kutoka Zanzibar, Salma Yusuph ambaye alichagua wimbo ambao kwa hakika ulikuwa umepooza mno kiasi cha kuruhusu mkoba huo akabidhiwe Walter, ambaye katika mashindano ya mwaka huu ameibuka kuwa kipenzi cha akina dada kutokana na sauti yake nyororo. Kila la Kheri Walter katika safari yako ya kimuziki. |
No comments:
Post a Comment