![]() |
| Askofu Methodius Kilaini. |
Askofu Msaidizi wa Kanisa Katoliki, Jimbo la Bukoba, Methodius Kilaini amekanusha habari iliyochapishwa na gazeti la Mwananchi katika toleo la jana kwamba aliiponda safu ya Uongozi na Sekretarieti ya CCM iliyoundwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete hivi karibuni.
Kupitia tamko lake kwa vyombo vya habari jana, Askofu Kilaini alisema amesikitishwa na habari hiyo iliyoandikwa na gazeti hilo. “Kwa masikitiko makubwa nimesoma katika gazeti la Mwananchi kwamba nimeiponda safu ya Uongozi na Sekretarieti ya CCM.
“Mimi sijaongea na gazeti lolote juu ya uongozi wa CCM na wala sina nia au sababu ya kuuponda uongozi huo. Ni vibaya kwa gazeti lolote lile kutumia jina la mtu kwa kueneza maoni yake. Kama ni waungwana natumaini watasahihisha waliyoyaandika. Nasikitika sana kwa waliokwazwa na hilo,” alisema Askofu Kilaini katika tamko lake hilo.
Katika uteuzi wa Sekretarieti ya CCM, Rais Kikwete alimteua, Abdulrahman Kinana kuwa Katibu Mkuu wa CCM, akisaidiwa na Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba upande wa Bara na Vuai Ali Vuai upande wa Zanzibar.
Wengine ni Zakhia Meghji aliyeteuliwa kuwa Katibu wa Uchumi na Fedha, Mohamed Seif Khatib (Oganaizesheni), Dk Rose Migiro (Kimataifa) na Nape Nnauye (Uenezi).
Uteuzi huo ulitanguliwa na uchaguzi ambao ulimrejesha Kikwete kuwa Mwenyekiti wa Chama wa Taifa akisaidiwa na Philip Mangula (Bara) na Dk Ali Mohamed Shein (Zanzibar).
Gazeti la Mwananchi liliripoti kwamba Askofu Kilaini alisema safu hiyo ya uongozi haina jipya akifafanua kuwa tatizo kubwa la chama hicho ni mfumo wake wa utendaji kazi.
“Ni mfumo ambao wamejiwekea wa kulindana, hivyo uongozi huu hautaleta mabadiliko yoyote CCM,” Gazeti hilo lilieleza kumnukuu Kilaini.
Kwa mujibu wa gazeti hilo, Kilaini alisema viongozi waliochaguliwa hawatakuwa na sauti kwa kuwa nao wana udhaifu wao, hivyo hawawezi kuwachukulia hatua wenzao kwa kuwa nao wataumbuliwa.
“Kati ya viongozi wa CCM waliochaguliwa hakuna atakayemnyooshea mwenzake kidole kwamba amefanya kosa fulani, ni vigumu mno kumwadhibu mwenzake kwa kuhofia kuwa kwa vile yeye pia ni dhaifu, akimwadhibu huyo matendo yake yatagundulika,” alidaiwa kusema.
Alidaiwa kusema pia kwamba licha ya Rais Kikwete kukemea rushwa kwa viongozi wote waliochaguliwa, lakini hakuna hatua yoyote aliyochukua kwa waliotuhumiwa kujihusisha na vitendo hivyo wakati wa uchaguzi wa ndani wa CCM.
“Rais wetu anazungumzia rushwa na kukemea, lakini hakuna aliyemchukulia hatua yoyote kwa waliokutwa wakitoa rushwa katika uchaguzi wa Umoja wa Vijana (UVCCM),” alinukuliwa Askofu Kilaini. Watu wengi wamekuwa na fikra tofauti juu ya uteuzi huo, baadhi wakiuunga mkono na kuupongeza na wengine wakiuponda.

No comments:
Post a Comment