| Kamanda Athuman Diwani. |
Mwenyekiti wa Chama cha Albino Tanzania (TAS) Mkoa wa Mbeya, Sinzo Dereva (38) ambaye ni mlemavu wa ngozi amenusurika kuuawa baada ya watu watano wasiofahamika kuvamia nyumbani kwake kwa nia ya kumfanyia uhalifu.
Akisimulia kisa hicho kwa njia ya simu kutoka wilayani Chunya jana, Dereva alidai tukio hilo lilitokea Oktoba mosi, usiku wa manane watu hao walipovunja nyumba anamokaa mama yake mzazi katika kijiji cha Magamba kata ya Songwe, Chunya.
Alidai kuwa walipoingia ndani ya nyumba hiyo, walimkamata mama yake na kumviringa kwenye godoro na kumfunga kamba baadaye wakafuata watoto na kuwalazimisha wawaoneshe alikojificha baba yao.
Watoto waliwasikia watu hao wakizungumza kwa lugha ya Kisukuma na kumtambua mmoja wao anayeishi katika kijiji jirani na chao.
Mmoja wa watoto wake aliwaambia kuwa baba yao alikuwa amesafiri wakati binti mkubwa aliwaambia kama walikuwa wakitaka pesa basi watawaonesha wapi bibi yao alikuwa akizificha – kwenye mfuko aliokuwa akiweka karanga.
Watu hao waliwapiga watoto hao kabla ya kutoka katika nyumba hiyo na kuwafungia kwa nje.
Dereva anasema watu hao walifanikiwa kuingia sebuleni mwa nyumba yake na kuhangaika kuvunja mlango wa kuingilia chumbani kwake. Hata hivyo, walihangaika kuuvunja mlango huo ambao ulikuwa ni imara kuliko milango yote kwenye nyumba hiyo. Walipogundua kuwa wasingeweza kuuvunja mlango huo, walizunguka nyuma na kujaribu kuingia ndani kupitia dirishani.
Hata hivyo, naye aliwasikia ‘wabaya’ wake wakizungumza kwa lugha ya Kiswahili na Kisukuma wakati wakielekezana nini cha kufanya. “Ujenzi wa nyumba yangu ulikuwa ukiendelea na dirisha la chumbani kwangu halikuwa limekamilika hivyo nilipanga matofali dirishani badala ya mbao na vioo,” alisema.
Hivyo walitumia udhaifu huo kusukuma matofali hayo ndani. Naye alichukua matofali hayo na kuwatupia kupitia dirishani huku akipiga kelele kuomba msaada. Pamoja na jitihada zake za kujiokoa, alijeruhiwa katika mkono wake wa kushoto na katika vidole vyake vya mkono wa kulia.
Dereva alitumia matofali hayo kupiga kwenye mabati ya nyumba yake kwa matumaini kuwa wanakijiji wenzake watasikia kelele hizo ili apate msaada.
“Nashukuru Mungu walisikia kelele hizo na walijitokeza kwa wingi. Watu watatu walikamatwa na wawili walitokomea gizani,” alisema na kuongeza kuwa Polisi Jamii hivi sasa wanampatia ulinzi anakoishi.
Dereva hata hivyo alisema ana uhakika waliokwenda kumshambulia ni wa kabila lake la Kisukuma wanaoishi wilayani humo. Alisema ndugu wa waliokamatwa wamekuwa wakimshawishi kufuta kesi na kwamba watampatia fedha kama wataachiwa ambapo alikataa na kutaka waache sheria ichukue mkondo wake.
Wakati huohuo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Athuman Diwani alikiri kwa njia ya simu kutoka mkoani humo kuwa tukio hilo lilitokea Oktoba mosi na kwamba watu watatu wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo na wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kutaka kufanya uhalifu.
Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Nzwano Mboje, Masanja Nzwano na Maige Isoda.
Dereva alihamia Chunya na mama yake akiwa na umri wa miaka mitano na ndugu zake watatu ambao si albino. Watu wengi wa kabila la Wasukuma wamekuwa wakihamia wilayani humo na wengine zaidi bado wanahamia.
Wilaya hiyo ni tajiri kwa madini ya dhahabu, ingawa wakazi wake wengi bado ni masikini.
Dereva ni mkulima wa mahindi na mtama kwa ajili ya chakula na ufuta kama zao la biashara. Hata hivyo, ana wasiwasi kwa kuwa kijijini hapo kuna watu wenye ulemavu huo wapatao 12, wanaume wakiwa ni sita na wanawake sita pia.

No comments:
Post a Comment