![]() |
| Shekhe Ponda Issa Ponda. |
Baada ya kusikika kwa muda mrefu akidaiwa kuhamasisha Waislamu kufanya vurugu na uvunjifu wa amani, huku akikwepa kutiwa nguvuni, hatimaye Shekhe maarufu Ponda Issa Ponda amenasa mtego wa Polisi.
Polisi jijini Dar es Salaam, inamshikilia Shekhe Ponda ambaye ni Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, pamoja na wafuasi wake 38, kwa tuhuma za uvamizi wa eneo, kufanya vurugu, uharibifu wa mali na uchochezi unaosababisha uvunjifu wa amani.
Aidha, imewataka wafuasi wengine wa Shekhe huyo waanze kujisalimisha kwa jeshi hilo mara moja, vinginevyo litawanasa katika mwendelezo wa operesheni maalumu ya kuwasaka popote walipo, kutokana na makosa mbalimbali ya jinai wanayodaiwa kutenda kwa vipindi tofauti.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema Shekhe Ponda amekuwa akisababisha vurugu nchini kila wakati na kuwakimbia polisi, lakini pamoja na kuwanyima usingizi mfululizo, usiku wa juzi walimtia mbaroni kirahisi.
“Kwa kuwa mbinu zake za kutukimbia tulikwishazifahamu tangu enzi zile za vurugu za Mwembechai, tuliamua kumtegea mtego uliomnasa ‘kilaini’ jana (juzi) saa 4 usiku, karibu na maficho yake. Ukamataji haukuwa wa madhara na aliletwa katika kituo hiki Kikuu cha Polisi kwa usafiri wa pikipiki,” alitamba Kova.
Kwa mujibu wa Kamanda huyo, pia wafuasi wa Shekhe Ponda waliokamatwa usiku wa kuamkia jana, wakiwamo wanawake saba wanaochukuliwa na Polisi kuwa wavamizi wa eneo walimkutwa, Chang’ombe Dar es Salaam, ambalo ni mali ya kampuni ya Agritanza.
“Ya Shekhe Ponda ni mengi, ndiyo maana tumeamua kuweka uvumilivu pembeni na kumkamata na wafuasi wake, ili atueleze anakopata kiburi na nguvu ya kutenda yasiyostahili kana kwamba yuko juu ya sheria. Amekuwa mstari wa mbele kutumia ‘vibaya’ Waislamu wanaomsikiliza, kutibua amani nchini,” alisema Kova.
Alitaja matukio ambayo Shekhe Ponda anatuhumiwa kuhusika nao na kushawishi wafuasi wake wayatende kuwa ni pamoja na vurugu za hivi karibuni Mbagala, Dar es Salaam, baada ya habari za mtoto wa miaka 14 kukojolea Kurani Tukufu kumfikia.
“Bila kujali kwamba taasisi anayoiongoza haijasajiliwa mahali popote, Shekhe Ponda amekuwa akiitumia kutekeleza jinai zenye hatari kwa Watanzania na mali zao. Amekuwa akiitumia kujikweza na kujipa nguvu za kimamlaka zaidi ya alizonazo Shekhe Mkuu wa Tanzania na Rais wa nchi, jambo tusilolikubali kimaadili na kisheria pia,” alisema Kova.
Aliendelea kutaja makosa mengine aliyohamasisha wafuasi wake wayatende kuwa ni kuvunja makanisa yasiyopungua manane Dar es Salaam wakati wa vurugu za kupinga kukojolewa Kurani Tukufu, kuharibu magari, vifaa vingine vya makanisa na wizi wa mali mbalimbali za watu.
Alisema Shekhe Ponda amekuwa akiongoza maandamano yasiyo na vibali katika maeneo mbalimbali ya nchi, hususan Dar es Salaam, huku akitanguliza mbele wanawake na watoto kukwepa mabomu ya kutoa machozi na vizuizi vingine vinavyoweza kutumiwa na Polisi kuyatawanya.
“Alifanya hivyo alipokwenda Wizara ya Mambo ya Ndani, Kidongo Chekundu na katika maeneo mengine. Halafu, bila kujua kwamba tumekuwa tukimsoma, amekuwa akijiona mshindi kwa kutamba mbele ya wafuasi wake kana kwamba Polisi inamgwaya wakati si kweli,” alisema.
Akizungumzia tukio la uvamizi wa kiwanja, Kamanda Kova alisema polisi walikesha kwa saa kadhaa katika maeneo ya karibu na kiwanja namba 311/3/4 kitalu T. Chang’ombe ambacho Shekhe huyo amekuwa akihamasisha ukombozi wake usio halali kupitia wafuasi wake na hivyo kusababisha vurugu na uvunjifu wa amani.
Kwa maelezo ya Kova, Oktoba 12, Shekhe Ponda aliongoza wafuasi wake ‘kuteka’ eneo hilo kwa madai ya kukomboa mali za Waislamu zilizouzwa isivyo halali na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) huku akijua kuwa anayelimiliki sasa (Agritanzi) alimilikishwa kihalali kwa kuzingatia utaratibu na kupewa na Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi hati namba 93773.
Katika uvamizi huo, Kamanda Kova alisema walikuta silaha za aina mbalimbali kama vile visu, mapanga, sururu na nyenzo tofauti za ujenzi, vinavyotunzwa na Jeshi hilo kama vielelezo vya ushahidi kesi itakapofikishwa mahakamani muda wowote baada ya mashitaka ya watuhumiwa hao kuthibitishwa na Wakili wa Serikali.
Mbali na hayo, Shekhe Ponda anashikiliwa kwa kuingilia uhuru wa Mahakama na kumtisha Rais Jakaya Kikwete kutokana na matamko yake yasiyofuata utaratibu, likiwamo lililomtaka awaachie walioshikiliwa na kufikishwa mahakamani kabla ya siku saba (kuanzia jana) kwisha.
“Amekuwa akitoa vitisho kwa taasisi mbalimbali pia kutokana na kukemea au kutomwunga mkono kwa mambo yake ya kuvuruga amani ya nchi, sasa hizo zote ni jinai ambazo Polisi kwa niaba ya umma halitazivumilia,” alisema.
Shekhe Ponda pia alipata kutajwa katika sakata la Waislamu kugomea Sensa ya Watu na Makazi mwaka huu.

No comments:
Post a Comment