Tuesday, October 9, 2012

CHEKA TARATIBU...

Mtaalamu wa lishe alikuwa akihutubia umati wa watu kwenye Viwanja vya Jangwani. Akasema, "Vitu tunavyoingiza tumboni vinatosha kabisa kuwa vimeshatuua wengi wetu miaka mingi iliyopita. Nyama nyekundu ni mbaya. Mboga za majani nazo ni balaa, na hakuna yeyote anayefahamu minyoo iliyomo kwenye maji tunayokunywa. Lakini kuna kitu kimoja ambacho ni hatari zaidi ambacho wote hapa huwa tunakula. Kuna yeyote anayeweza kunitajia ni kipi hicho? Enhe, hapo mzee mstari wa kwanza, tafadhali tutajie!"
Huku akiinamisha kichwa chake mzee akajibu, "Keki ya Harusi!" Balaa...

No comments: