CHEKA TARATIBU...

Ili jamaa watatu waliopanga chumba katika ghorofa ya 60 kwenye hoteli moja wasione uvivu wakati wakipanda ngazi, wakakubaliana wasimuliane hadithi kama ifuatavyo. Mmoja asimulie hadithi ya furaha hadi ghorofa ya 20, mwingine asimulie hadithi ya kutisha hadi ghorofa ya 40 na mwingine asimulie hadithi ya kuhuzunisha hadi ghorofa ya 60. Basi wakaanza kupandisha ngazi na walipofika ghorofa ya 59, jamaa wa tatu akasema "hadithi yangu ya kuhuzunisha inaishia hivi kwamba TUMESAHAU UFUNGUO WA CHUMBA PALE MAPOKEZI GHOROFA YA CHINI! Duh…

No comments: