CHEKA TARATIBU...

Bosi mmoja alikuwa akiendesha gari kwa kasi katika kijiji kimoja. Ghafla akagonga mbuzi na kumuua. Baada ya kuzozana na mwenye mbuzi kwa muda, yule Bosi akauliza, "Nataka kujua thamani ya huyu mbuzi." Mmiliki akajibu, "Shilingi elfu hamsini! Lakini baada ya miaka kumi atafikia thamani ya Shilingi milioni mbili. Hivyo nataka unilipe fidia ya Shilingi milioni mbili!" Bosi akafungua mkoba wake na kuandika hundi ya kiasi hicho lakini ya tarehe ya mbele ya miaka 10! Duh

No comments: