POLISI 'WASHIKWA GANZI' MAANDAMANO YA WAISLAMU KIDONGO CHEKUNDU...

Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wakiwa ameegesha magari yao katika kiwanja cha Kidongo Chekundu huku wakiwa hawajui wawafanye nini waumini wa madhehebu ya Kiislamu waliokaidi zuio la kukusanyika katika kiwanja hicho jana.
Maelfu ya waumini wa madhehebu ya Kiislamu wakiwa wameshikilia mabango yao kuilaani Marekani wakati wa maandamano yao yaliyoishia kiwanja cha cha Kidongo Chekundu, Dar es Salaam jana .
Licha ya Polisi kupiga marufuku mkutano wa Waislamu, baadhi ya waumini wa dini hiyo walio chini ya Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, jana wamefanya mkutano huo huku wakisisitiza kutekeleza azma yao kumng’oa madarakani Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Issa bin Shaaban Simba.
Katika mkutano huo uliofanyika katika kiwanja cha Kidongo Chekundu chini ya ulinzi mkali wa Polisi, Katibu Mkuu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Issa Ponda, mbali na azma hiyo, pia wamekusudia kufanya maandamano hadi Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) kwa ajili ya kumtoa madarakani Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Dk. Joyce Ndalichako.
Huku wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe mbalimbali yakiwemo yanayosomeka ‘Kwa nini wanamchukia Mtume Muhammad (S.A.W) Uislam ni dini ya kweli’ ‘Mtume Muhammad mkweli na mwaminifu’ na mengineyo, wamesisitiza kutonyamaza kimya dhidi ya watu wote wanaomkashifu kiongozi huyo.
Akisoma tamko katika Mkutano huo ulioanza Saa 7 mchana hadi Saa 11 jioni, Sheikh Ponda, pia ameitaka Serikali kuuondoa Ubalozi wa Marekani hapa nchini kwa madai kuwa nchi hiyo imekuwa ikifanya vitendo vya kidhalimu dhidi ya waumini wa dini ya Kiislamu hapa nchini.
Katika tamko hilo Sheikh Ponda amesema waislamu nchini wanalaani watu walioitengeneza filamu hiyo huku wakiitaka Serikali kupiga marufuku mitandao yote kuendelea kuionyesha filamu hiyo pamoja na kuishinikiza Marekani kuwachukulia hatua kali watu waliohusika katika utengenezaji wake.
"Pamoja na maneno yote yanayoongelewa, lengo la kumng’oa Mufti lipo pale pale, Bakwata pia, tunataka haki kwa waislamu, siku zao zinahesabika hakuna kulala mpaka kieleweke," alisema Sheikh Ponda.
Hata hivyo, tamko hilo linakuja siku tatu baada ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania kupitia kwa Kiongozi wake Sheikh Issa bin Shaaban Simba kutoa tamko lao kupinga utengenezwaji wa filamu hiyo.
Akiizungumzia filamu hiyo, Ponda alisema ililenga kupandikiza chuki kwa waislamu dhidi ya Mataifa mbalimbali sambamba na kumdalilisha kiongozi wao Mtume Muhammad (S.A.W) suala alilosema kamwe haliwezi kunyamaziwa na waumini wa dini hapa duniani kote.
Awali wakitoa mada katika mkutano huo, Masheikh kutoka Misikiti mbalimbali Jijini Dar es Salaam akiwemo wa msikiti wa Idrissa uliopo Kariakoo, Ali Bisalala, alisema linapofika suala la kuitetea dini hiyo, watahangaika hadi pale haki inapopatikana.
Akitolea mfano wa mkutano huo ambao awali ulizuiwa na Polisi kabla ya kufanikiwa kufanyika baadae, Sheikh Bisalala alisema lengo la waislamu si kuleta vurugu isipokuwa wanalazimishwa kufanya hivyo pale wanapoona haki zao zinakandamizwa.
Mkutano huo uliolenga kuipinga filamu hiyo inayodaiwa kuudhalilisha Mtume pamoja na waumini wote wa dini ya Kiislamu, umefanyika kwa amani huku magari ya polisi zaidi ya manane yaliyosheheni polisi, gari lililobeba maji ya kuwasha, na askari waliovalia kiraia wakizunguka kulinda amani katika eneo hilo.

1 comment:

Anonymous said...

Naomba kujua ukweli juu ya malumbano haya

vsaluki • Let's keep telling the truth about Islam. If the Muslims don't like it, too bad. They choose the prophet of violence and the religion of violence. It is their problem, not ours. We should never allow ourselves to be intimidated into silence by seventh century thugs.
2 Replies
o moe • 11 hrs ago
her and prayed for her when she was sick. He forgave all the Meccans who had tortured him and his followers all the time.He was a man of Mercy. You are misguided He and his people had to fight to protect their lives and properties.
He never initiated a war or fight. They were all defensive fights.You must first
learn the You are the most ignorant!!! Prophet Muhamma[peace be upon him] was the most compassionate. He was thrown into the desert for three years. He alsways prayed for them. A Jewish woman threw garbage on him. He never complained. He visied basics of Islam. I am sure you will change your views.
o vsaluki • 11 hrs ago
Moe: "Prophet Muhamma[peace be upon him] was the most compassionate."

You are lying. Mohammed was a murderer, a liar, a rapist, a sexist, a bigot, a caravan robber, a pedophile, a slave trader and a war monger.

He led 17 major military expeditions and the majority of them were offensive, not defensive. He called the Jews apes and pigs in Quran 5.60. He told men that they could beat women in Quran 4:34. He gave women half the rights of men in court in Quran 2:282. He permitted the rape of slave girls in Quran 23.1-6 and Quran 7.30. And he told Muslims to attack non Muslims until they were subjugated.

[9.29] Fight those who do not believe in Allah, nor in the latter day, nor do they prohibit what Allah and His Apostle have prohibited, nor follow the religion of truth, out of those who have been given the Book, until they pay the tax in acknowledgment of superiority and they are in a state of subjection.

[8.39] And fight with them until there is no more persecution and *** religion should be only for Allah;*** but if they desist, then surely Allah sees what they do.
o GXtro • 7 hrs ago@Moe. are you for real. You cannot not truly be that STUPID can you ?
o