Mkuu Mpya wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Samwel Ndomba, akila kiapo mbele ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi. Meja Jenerali Ndomba anachukua nafasi ya Meja Jenerali Samwel Kitundu, aliyestaafu hivi karibuni kwa mujibu wa sheria. (Picha na Freddy Maro)
Rais Jakaya Kikwete ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu, amemteua Meja Jenerali Samuel Ndomba kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).Aidha, Rais Kikwete amempandisha cheo Meja Jenerali Ndomba kuwa Luteni Jenerali.
Taarifa iliyotolewa jana jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais – Ikulu, imesema kuwa uteuzi huo umeanza mara moja.
Taarifa hiyo ya Balozi Sefue imesema kuwa kabla ya uteuzi wake, Meja Jenerali Ndomba alikuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT). Anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Luteni Jenerali Abdulrahman Shimbo ambaye amestaafu Jeshi kwa mujibu wa sheria baada ya kufikisha umri wa miaka 60.
Rais Kikwete pia amemteua Brigedia Jenerali Raphael Muhuga kuwa Mkuu wa JKT kuanzia jana.
No comments:
Post a Comment