CHEKA TARATIBU...

Jamaa kaingia kwenye baa na kukuta rafiki yake akinywa peke yake katika meza iliyoko kwenye kona kabisa. Baada ya salamu jamaa akauliza, "Unaonekana huna furaha, nini tatizo?" Rafiki akajibu:
"Mama yangu amefariki Agosti na kuniachia Shilingi milioni 25."
Jamaa akajibu, "Pole sana."
"Kisha Septemba, kafariki baba yangu akaniachia Shilingi milioni 30."
Jamaa akajibu, "Duh, wazazi wote wawili wamekutoka ndani ya miezi miwili. Haishangazi kuona una huzuni hivyo."
"Na mwezi uliopita, shangazi yangu naye akafariki na kuniachia Shilingi milioni 15."
Jamaa akasema, "Ndugu watatu wa karibu wamekutoka katika miezi mitatu? Huzuni kubwa hiyo."
"Sasa mwezi huu," akaendelea yule rafiki, "nimechacha ile mbaya sina hata senti moja!" Duh...

No comments: