CHEKA TARATIBU...

Fundi seremala kata oda ya kutengeneza jeneza. Ili aweze kuendelea kupata tenda nyingi iwezekanavyo, akaamua kujitolea zaidi ili kutengeneza jina mitaani. Alipomaliza akalipakia kwenye gari lake na kuanza safari ya kulipeleka kwa wafiwa ili aweze kumaliziwa pesa yake iliyobakia. Akiwa njiani gari likaharibika, hivyo akaamua kujitwisha na kuanza kutembea nalo kwa miguu akikatisha eneo la Kinondoni Makaburini jioni kabisa. Mara akakutana na polisi wa doria wakamsimamisha na kuanza kumhoji alikolitoa lile jeneza na wapi analipeleka. Haraka akajua wale polisi wanachotaka ndipo akajibu kwa kujiamini, "Walinizika hapo Kinondoni, lakini sikupapenda. Sasa niko njiani kwenda Sinza!" Duh, kusikia vile, polisi wote wakatoka mkuku kila mmoja upande wake...

No comments: