DARASA LA SABA WAANZA MITIHANI YAO YA MWISHO LEO...

Jumla ya wanafunzi 894,881 wa Darasa la Saba wa shule zote sehemu mbalimbali hapa nchini leo watarajiwa kuanza mitihani yao ya mwisho ya kumaliza elimu ya msingi.
Mitihani hiyo inafanyika huku shule nyingi zikikabiliwa na changamoto za ukosefu wa madawati na hivyo kulazimu wanafunzi  kufanya mitihani hiyo wakiwa wamepakata karatasi za maswali miguuni mwao huku wakiwa wameketi sakafuni.
Pamoja na hayo, Mhariri wa "ziro99blog" anawatakia wanafunzi wote kila la kheri katika kufanya vema mitihani hiyo na wasimamizi wote wa mitihani hiyo umakini mkubwa ili taifa liweze kupata wanafunzi bora ambao watakuja kuwa wataalamu kwenye nyanja mbalimbali katika miaka kadhaa ijayo.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika!

No comments: