AOKOLEWA NA PAPA BAADA YA KUPOTEA BAHARINI KWA SIKU 106...

Mtu ambaye aliyenusurika wakati akielea ovyo kwenye bahari ya Pacific kwa siku 106 amemsifu papa kwa kusaidia kuokoa maisha yake.
Toakai Teitoi mwenye miaka 41, askari polisi kutoka kisiwa cha Central Pacific taifa la Kiribati, alikuwa akisafiri na shemeji yake wa kiume katika kile kilichofahamika kama safari fupi, iliyoanza Mei 27, kutoka mji mkuu wa Kiribati, Tarawa kuelekea kisiwa yaliko makazi yao cha Maiana.
Lakini waongoza meli hao waliamua kuvua samaki safarini, na kupitiwa usingizi wakati wa usiku. Walipoamka walikuwa mbali mno katika bahari hiyo na kupoteza mwelekeo wa chombo chao hicho chenye ukubwa wa futi 15. Baada ya muda mfupi wakaishiwa mafuta.
"Tulikuwa na chakula, lakini tatizo likawa hatuna cha kunywa," Teitoi alieleza Shirika la Habari la Agence France-Presse.
Ukosefu wa maji mwilini ulikuwa mkali mno. Falaile, shemeji mwenye miaka 52, alifariki Julai 4. Usiku huo, Teitoi alilala kando yake, "kana ilivyo kwenye msiba," kabla ya maziko yenye hisia katika bahari asubuhi iliyofuata.
Teitoi amesimulia mkasa huo baada ya kusawili mjini Majuro, kwenye Visiwa vya Marshall, Jumamosi iliyopita. Alisema alisali usiku huo ambao Falaile alifariki, na siku iliyofuata kimbunga kilipiga eneo hilo na, kwa siku kadhaa zilizofuata, alimudu kuweza kujaza maji safi kwenye galoni mbili zenye ujazo wa lita tano kila moja.
Siku na wiki zilipita, hatahivyo, na Teioti, baba wa watoto sita, hakuweza kujua kama atakuwa hai au kufa. Alijikimu zaidi kwa samaki na kujikinga dhidi ya jua kali baharini kwa kujibanza kwenye kijisehemu kidogo cha upinde.
Ilikuwa mchana wa Septemba 11 ambao aliamshwa na mlio wa mkwaruzo kwenye boti yake. Papa mwenye urefu wa futi sita alikuwa akikokota boti na, Teitoi alisema, kwa kutumia magamba yake.
"Alikuwa akiniongoza kuelekea iliko boti ya uvuvi," Teitoi alisema. "Nilitazama na kulikuwa na meli na nikaweza kuona mabaharia wakinitazama kwa kutumia darubini."
Kitu cha kwanza alichoniulizwa baada ya kutolewa kwenye maji ni sigara, au "chochote cha mfano huo." Alipatia chakula na juisi na waokozi wake waliendelea kuvua samaki kwa siku kadhaa kabla ya kumkabidhi Majuro.
Teitoi, ambaye alionekana mwenye afya njema, alisema alikata tiketi ya ndege kurejea kisiwani yaliko makazi yake, akiongezea, "Siendi tena kwa kutumia boti."

Rekodi ya kuelea ovyo baharini humo inaaminika kushikiliwa na wavuvi wawili pia kutoka Kiribati, ambao walikaa baharini kwa siku 177 kabla ya kufika ufukweni huko Samoa mwaka 1992.

No comments: