CHEKA TARATIBU...

Kipofu mmoja alipata ofa ya kutembelea Afrika Kusini. Alipofika kwenye ndege, akapapasa kiti na kusema, " He, hivi viti ni vikubwa mno!" Abiria aliyekuwa pembeni yake akamjibu, "Kila kitu ni kikubwa Afrika Kusini."
Mara alipofika Afrika Kusini, akaamua kwenda baa. Alipowasili tu, akaagiza bia na kuwekewa chupa katikati ya mikono yake. Akasema, "He, hii chupa ni kubwa mno!" Mhudumu akajibu, "Kila kitu ni kikubwa Afrika Kusini."
Baada ya kunywa bia kadhaa, yule kipofu akamuuliza mhudumu kilipo choo. Mhudumu akajibu, "Mlango wa pili kulia." Kipofu akaelekea huko, lakini kwa bahati mbaya akaupita mlango wa pili. Badala yake akaingia wa tatu akatokea kwenye bwawa la kuogelea na kutumbukia bwawani kwa bahati mbaya.
Akihofia kifo kwa kudhani katumbukia chooni, kipofu akaanza kupiga kelele, "Usiflashi, usiflashi tafadhali!" Balaa...

No comments: