AGUNDUA MUMEWE ALIKUWA NI BABA YAKE MZAZI...

Mwanamke amezungumzia tukio la kutisha kufuatia kugundua mwishoni kwamba mumewe aliyefariki alikuwa ni baba yake mzazi.
Valerie Spruill mwenye miaka 60 mkazi wa Doylestown, mjini Ohio, ameweza kufanya ugunduzi huo kupitia kipimo cha DNA baada ya mumewe Percy kuwa amefariki dunia.
Valerie, ambaye ana watoto watatu na wajukuu nane, sasa anaelezea mkasa wake huo katika kile alichoelezea ni kutafuta ndugu zake wengine kwa baba yake huyo.
"Inalazimu kuzungumziwa, sababu watoto wanahitajika kujua wametokea wapi," alilieleza Jarida la Akron Beacon. "Na nafahamu inaumiza, sababu nimekuwa nikiteketezwa na hili."
Utata ulianza sababu alikuwa akilelewa na babu yake tangu akiwa na umri wa miezi mitatu.
Mama yake Christine alikuwa mmojawapo wa 'machangudoa' - kama alivyowaita - ambaye alitoa ushahidi katika kesi ya mwaka 1980 iliyokuwa ikimkabili Jaji James Barbuto, ambaye baadaye alitiwa hatiani kwa mashitaka ya ubakaji.
Mama wa Valerie na baba yake walianza kuishi pamoja wakati baba huyo akiwa na miaka 15 tu na idada ya watoto haijulikani, lakini anawatambua kaka zake sita pekee.
Alilelewa na babu na bibi yake huku mama yake akimtembelea, ingawa Valerie alidhani kuwa ni rafiki wa familia hiyo.
Akiwa na miaka tisa, alipagawa pale alipogundua kwamba Christine - ambaye alifariki mwaka 1984 - alikuwa ni mama yake mzazi. Hiyo ilimaanisha pia kwamba mwanaume ambaye alikuwa akidhani kuwa ni baba yake kumbe ni babu yake.
Lakini hakuelezwa nani hasa alikuwa baba yake mzazi na Valerie baadaye akakutana na kufunga ndoa na Percy.
Percy, ambaye alizaliwa huko Mississippi, alikuwa akifanyakazi kama dereva wa malori na mwangalizi wa eneo la maegesho.
Alifariki dunia mwaka 1998 baada ya kuugua kwa muda mfupi akiwa na umri wa miaka 60, lakini kwa miaka kadhaa, alisikia uvumi usio wa kawaida kuhusu mahusiano yao.
Valerie hatimaye akapata ukweli kuhusu ndoa yake kutoka mjomba wake baada ya kifo cha Percy, na kuthibitisha mahusiano yao kwa kipimo cha DNA baada ya kukuta nywele zake katika brashi chumbani kwao.
Hakujua mara moja kama alikuwa anajua kwamba amemuoa binti yake, lakini alisema anaamini kabisa Percy alijua lakini alikuwa anaogopa kumweleza.
Tangu kifo chake, Valerie, ambaye amestaafu, amekuwa akienda kwa wataalamu kusaidia mpango wake huo wa ufunuo wa kuogopesha.
Valerie amepitia katika mapambano makubwa ya matatizo ya kiafya, ikiwamo kulazwa kwa muda mrefu hospitalini, ambayo anaamini ilisababishwa na msongo wa mawazo kufuatia kugundua siri kubwa ya familia.
Anaamini stori yake inaweza kusaidia kuwapata ndugu zake zaidi waliopo ambao hawajui.
"Mafanikio yangu mwakubwa ni kuwapata na kuwafanya wafahamu kwamba (mama yao) aliwapenda sana, bila kujali chochote," alisema Valerie.

No comments: