CHEKA TARATIBU...

Mume mmoja alikuwa na desturi ya kunywa glasi moja ya wiski kila siku kabla ya kulala. Baada ya miaka kadhaa ya kufanya hivi, ndipo mkewe akaanza harakati za kukomesha tabia hiyo. Akachukua glasi mbili, moja akaweka wiski na nyingine maji. Akaziweka mezani kisha kamwita mumewe na kuanza kumpatia somo, "Nataka utazame hiki." Akaweka minyoo katika glasi ya maji, ikawa inatembea huku na kule kwenye maji. Akaweka minyoo katika glasi ya wiski, ile minyoo ikafa pale pale. Huku akidhani somo limeeleweka vizuri mke akauliza, "Umejifunza nini kuhusu hiki nilichokuonesha?" Mume kwa umakini akajibu, "Kama nikinywa wiski, kamwe siwezi kupata minyoo!" Kasheshe...

No comments: