NYOTA WA RUGBY AZAMA NA KUFA AKIJARIBU KUOKOA NDUGU ZAKE TOPENI...

Mchezaji rugby wa kulipwa amekufa mbele ya baba na kaka yake baada ya kutumbukia kwenye tope laini katika shamba lao la familia.
Nevin Spence mwenye miaka 22, na kaka yake Graham mwenye miaka 30, walikumbana na harufu kali wakati wakijaribu kumwokoa baba yao Noel mwenye miaka 52, kutoka kwenye tope lililokuwa shambani huko mjini Co Down, Ireland ya Kaskazini.
Dada wa Nevine, Emma, ambaye pia alijaribu kusaidia, alijikuta katika wakati mgumu na kukimbizwa hospitalini kwa matibabu.
Imefahamika kwamba Noel alitumbukia muda mrefu kabla wakati alipokuwa akijaribu kumwokoa mbwa wao aliyekuwa kanasa kwenye tope laini.
Nyota wa michezo wakiwamo Rorry McIlroy wametuma salamu za rambirambi kwa mchezaji huyo wa timu ya Ulster.
Kikosi cha wafanyakazi wa dharura kilifika katika shamba hilo la familia lililoko Barabara ya Drumlough, nje ya Hillsborough, mjini Co Down, muda mfupi baada ya Saa 12 jioni ya Jumamosi kufuatia ripoti kuwa watu wanne wametumbukia kwenye tope laini.
Wawili kati yao walisemekana kufa katika eneo la tukio lakini wafanyakazi wa uokoaji waliweza kumvuta mwanaume na mwanamke.
Madaktari hawakuweza kuokoa maisha ya mwanaume. Mwanzoni alionekana kupata nafuu kufuatia juhudi za kunusuru maisha yake na alipelekwa katika Hospitali ya karibu ya Lagan Valley iliyoko mjini Lisburn, lakini alitangazwa kufariki muda mfupi baada ya kufikishwa hapo.
Afya ya Emma juzi iliimarika katika Hospitali ya Royal Victoria mjini Belfast, ambako alikuwa akipatiwa matibabu kutokana na athari za kuvuta harufu kali.
Emma ni mchoraji ambaye miongoni mwa kazi zake alizowahi kufanya ni picha za sura za wachezaji wa Ulster.
Askari mmoja wa kikosi cha zimamoto aliyejitosa kwenye shimo kujaribu kunusuru, na alikuwa akipatiwa matibabu kutokana na uwezekano wa kuwa alipata maradhi juzi usiku.
Uchunguzi kujua sababu ya ajali hiyo unaendelea lakini kuna ripoti ambazo hazijathibitishwa kwamba wanafamilia hao walikuwa wakijaribu kumwokoa mbwa wao aliyekuwa katumbukia kwenye shimo, kabla Nevin kujitosa kusaidia kuwaokoa ndugu zake.

No comments: