CHEKA TARATIBU...

Wakiwa wamefikia mwisho wa usaili wa kazi, Ofisa Rasilimali Watu akamuuliza Mhitimu wa Chuo Kikuu aliyekuwa akisailiwa, "Unataka tukulipe mshahara kiasi gani wa kuanzia?"
Mhitimu akajibu, "Kiasi chochote kile lakini sio chini ya Shilingi milioni 10 kwa mwezi kutegemeana na marupurupu yatakayoambatana na mshahara huo."
Ofisa akasema, "Vizuri, utasemaje tukikupatia marupurupu ya Liziko za wiki tano mara sita kwa mwaka, Mapumziko 14 yaliyolipiwa, Huduma za Matibabu kwa Ukoo wako wote, Asilimia 50 ya jumla mishahara yako kwa miaka utakayofanya kazi wakati wa kustaafu, Kukununulia gari moja kila mwaka, Kukununulia nyumba maeneo ya Masaki?"
Mhitimu akasimama ghafla na kusema, "Ebo! Unafanya utani?"
Ofisa akasema kwa upole, "Bila shaka ...lakini wewe ndio uliyeanza!"

No comments: