Eneo ambako unyama huo ulifanyika.
Mwanamke alikabiliwa na mateso yaliyodumu kwa masaa sita baada ya kutekwa nyara, kuzibwa mdomo na kisha kubakwa katika gari lililogeuzwa 'gereza linalotembea'.Mwanamke huyo mwenye miaka 24 alisema alihofia maisha yake baada ya kuwa ametekwa huku akitishiwa kisu na mtu aliyehusika katika matukio kadhaa ya ubakaji, Kevin John Hills.
Kevin mwenye miaka 40, ambaye alihukumiwa kifungo cha miaka tisa, alikuwa nje kwa dhamana kwa kosa la kusambaza picha za watoto wakijihusisha na vitendo vya ngono wakati wa tukio hilo la utekaji nyara.
Mwanamke huyo alikutana na Kevin katika eneo la Highfields, huko Leicester ambako anafanya kazi kama kahaba.
Wakati alipokuwa akimfuata Kevin kwenye gari, alimtolea kisu na kumlazimisha kuingia kwenye gari, mahakama ya Leicester ilielezwa.
Baada ya kuona msumbufu wake akifungwa jela, muathirika huyo alisema anakumbuka mara kwa mara shambulio na bado analifikiria karibu kila siku.
"Imeharibu maisha yangu. Siwezi kukaa peke yangu, najihisi siko salama na kuhofia wakati wote, lakini najitahidi kujaribu kupambana na kivuli hicho cha kutisha alichosababisha mtu huyo maishani mwangu.
"Hukumu hiyo inatosha lakini natamani kama angekaa jela milele. Namchukia mno. Hakika nilidhani naelekea kufa."
Baada ya kufungwa mikono yake na mdomo kuzibwa kwa gundi ya karatasi, mwanamke huyo alijaribu kutaka kujirusha kutoka kwenye gari hilo lililokuwa kwenye mwendo mkali, lakini Kevin alisema: "Endelea kukaa. Sipati hasara yoyote kama utakufa ama kubaki hai."
Jaji Sylvia De Bertodano alisema: "Ni kitu ambacho hakuna mtu anayependa kimtokee."
Kevin, anayetokea huko Beumont Leys, mjini Leicester alimvutia kwenye gari, akampiga maeneo mbalimbali kichwani na kumparura miguuni, kabla ya kumpeleka kwenye eneo lililojitenga karibu na Ziwa Cropston.
No comments:
Post a Comment