Wednesday, August 15, 2012

VAN DAMME AKIRI KUFANYA MAPENZI NA MWIMBAJI KYLIE MINOGUE...

Anaweza kuonekana kuwa mwenye furaha sana wakati akiwa ametulizana na mkewe kwenye Uzinduzi wa filamu ya Expendables 2 mjini London, lakini kunaweza kukawepo kitu ambacho Gladys Portugues hakifahamu kuhusu Jean-Claude Van Damme.
Mwigizaji huyo mwenye miaka 51 hivi karibuni alikiri kwamba alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na nyota wa muziki wa Pop, Kylie Minogue mwaka 1994.
Katika mahojiano na gazeti la The Guardian, ambako mwigizaji huyo alipromoti filamu yake mpya, katika hali ambayo haikutarajiwa aliamua kuweka wazi jambo hilo.
"Nakueleza nini, unatakiwa kumuuliza yeye (Kylie). Anaweza kuwa na kumbukumbu nzuri," alilieleza gazeti hilo. "Nina miaka 51, unaweza kujua nimedundwa mara ngapi usoni katika The Expendables? Hapana. Hivyo wacha tuseme imeshatokea, nini cha zaidi? Nani anataka kujua?
"Sawa. Ndio. Imeshatokea. Nilikuwa Thailand, tulikuwa na mahusiano ya kimapenzi."
Inaonesha mahusiano kati ya wapenzi hao yalikuja wakati Jean-Claude na Kylie wakitengeneza filamu ya Street Fighter, na kwa mujibu wake, haikuweza kuepukika.
"Busu mwanana, mapenzi motomoto," aliongeza. "Ingekuwa si kitu cha kawaida kama nisingeanzisha mahusiano, ni mrembo sana na alikuwapo mbele yangu kila siku akiwa na tabasamu murua, lenye kusisimua, mcheshi mno, alikuwa haigizi kama nyota mkubwa.
"Niliifahamu Thailand vizuri sana, hivyo nilimwonesha Thailand yangu. Alikuwa msichana wa kipekee."
Filamu hiyo ya mikikimikiki iliingia sokoni mwaka 1994, lakini hakufahamika wazi upigaji picha ulifanyika lini hasa.
Jean-Claude na Gladys hawakuwa wakiishi pamoja kwa wakati huo na kwamba walitengana mwaka 1992 baada ya ndoa yao iliyodumu kwa miaka mitano na wakarudia kuoana mwaka 1999.
Hata hivyo, wakati wakiwa wametengana, Jean-Claude alimuoa Darcy LaPier mwaka 1994.

No comments: