Stallone alijitokeza hadharani jana wakati akipromoti filamu yake mpya ya 'The Expendables' …ndipo waandishi walipomuuliza maisha yake yalivyo tangu kufariki kwa Sage mwezi uliopita.
"Ni magumu ni magumu mno," Stallone alisema …akaongeza, "Lakini ukiwa na marafiki wazuri na msaada kutoka kwa familia, ni jambo fulani la kutisha lakini …natumaini inatibika na unajaribu kuachana nayo lakini ni jambo ambalo lipo katika maisha."
Stallone alisisitiza kwamba kutengeneza filamu yake mpya kumemsaidia kusahau machungu …akisema, "Ni muhimu kurudi nyuma na kujaribu kuanza kuishi upya maisha yako, vinginevyo unaweza kuishia katika mzunguko."
Sage, ambaye alicheza kwenye filamu ya "Rocky 5" sambamba na Sylvester, alifariki dunia Julai 13, mwaka huu kutokana na kujizidishia dozi ya dawa. Alikuwa na umri wa miaka 36.
No comments:
Post a Comment