Mwanamke aliyeachwa akihitaji msaada wa kiti cha magurudumu kuweka kutembea kufuatia kushambuliwa mtaani hawezi kupata haki yake baada ya mkanganyiko kati ya polisi na waendesha mashitaka kuruhusu mtu huyo kukwepa mkono wa mahakama.
Nikki Brewer mwenye miaka 21, alikuwa akitembea kuelekea nyumbani akiwa na rafiki yake katika matembezi ya usiku ndipo alipovamiwa na mtu mmoja aliyelewa.
Picha za kamera ya CCTV zimemuonesha mtu huyo akimvuta nywele mwanamke huyo na kumbinua kichwa chake kwa nyuma kabla ya kumshindilia konde la nguvu lililomdondosha chini huko Colshester.
Nikki sasa anasumbuliwa na maumivu ya kudumu ya uti wa mgongo na anahitaji kiti maalumu cha magurudumu kumwezesha kutembea. Madaktari wamemchunguza na kugundua maradhi yaliyoathiri mishipa yake ya fahamu ambayo yanawezekana kabisa kusababishwa na majeraha aliyopata.
Polisi waliomba mashahidi kujitokeza na mtu huyo mwenye miaka 31 alikamatwa Januari mwaka huu kwa shambulio la kudhuru mwili.
Lakini sasa tayari ameelezwa hatoweza kushitakiwa kutokana na kushindwa kufikishwa mahakamani kwa kipindi cha miezi sita muda ambao kisheria mtuhumiwa anatakiwa kuwa ameshafanyiwa hivyo.
Endapo angetuhumiwa kwa makosa zaidi ya kudhuru, kama kudhuru mwili, hakuna muda wa mwisho ambao ungemnusuru na mashitaka.
Sababu hasa ya kuchelewa ilibainishwa ni mkanganyiko juzi huku Polisi wa Essex na Waendesha mashitaka kulaumiana kila mmoja kwa kushindwa kuchukua hatua.
Polisi wamesema walipepewa ushauri na Waendesha mashitaka kwamba majeraha ya Nikki hayakuwa makubwa kuweza kutoa notisi ya kukamatwa mtuhumiwa kwa ajili ya mashitaka ya kudhuru.
Pia ilidaiwa Waendesha mashitaka waliamua kutoendelea na kesi lakini Ofisi ilijibu kwa kusema haikuwahi kushughulikia faili lenye ushahidi.
"Mtu huyu bado yuko huko nje na anaweza kufanya kitu hicho hicho kwa mtu mwingine," alisema Nikki, mfanyakazi wa Idara ya Utawala katika Kituo cha Multiple Sclerosis kilicho karibu na mahali anapoishi. "Inachanganya sana kuona mtu huyo anatembea akiwa huru kabisa."
Nikki, ambaye ameolewa na Mratibu wa Masuala ya Upasuaji, Lee mwenye miaka 22, alikuwa na miaka 18 wakati aliposhambuliwa kwenye mtaa wa Colchester Aprili 2009. Mtuhumiwa alimtisha kwanza rafiki wa Nikki na alipofanikiwa kukimbia ndipo alipomvamia mwanamke huyo na kumshambulia.
Mwanaume mwingine eneo la tukio aliyevalia nguo zinazoooneka kama rangi ya machungwa, imeelezwa kuwa ni rafiki wa mtuhumiwa huyo. Hakutoa msaada wowote.
Nikki anasumbuliwa na maumivu ya mgongo na jicho lake limevilia damu. Lakini madaktari baada ye waligundua hali inayoendelea kwamba anawezekana kuwa amedhurika zaidi katika tukio hilo.
Kufuatia shambulio hilo, sasa analazimika kutembea kwa kutumia kiti chenye magurudumu ili kupunguza mgandamizo kwenye uti wa mgongo.
Nikki pia aliwashutumu polisi kwa kushindwa kuchukua hatu haraka vya kutosha sababu waliomba ushahidi kwenye runinga pekee Septemba 2010.
Polisi wamesema ofisi ya mwendesha mashitaka imeamua kutoendelea na kesi. Msemaji aliongeza, "Mtuhumiwa wa shambulio hilo alikamatwa na kuachiwa kwa dhamana na polisi."

No comments:
Post a Comment