Kamanda wa Polisi, Zelothe Steven.
Mwanafunzi wa darasa la saba Shule ya Msingi Hogolo, wa umri wa miaka 14 (jina limehifadhiwa) ambaye ni mkazi wa Mtaa wa Ikulu Kijiji cha Hogolo wilayani Kongwa, ameuawa kwa kunyongwa na kuzikwa kwenye shimo nyuma ya nyumba yao karibu na choo baada ya kubakwa.Uchunguzi wa awali unaonesha kuwa chanzo cha mauaji hayo yaliyofanyika Jumamosi iliyopita ni wivu wa kimapenzi, kwani marehemu enzi za uhai wake, anadaiwa alikuwa amevunja uhusiano na mpenzi wake wa muda mrefu, Heri Aboubakar na kuanzisha uhusiano mpya na Wilfredy Muhaha maarufu Kabo.
Hata hivyo, haijafahamika muuaji halisi wa mwanafunzi huyo licha ya polisi kuwashikilia watu kadhaa kwa tuhuma za kuhusika na tukio hilo akiwemo mpenzi wake wa sasa, Muhaha.
Mbali na Muhaha, wengine wanaoshikiliwa Polisi ni Ashad Jafari ambaye ni mkulima na mkazi wa Mtaa wa Nyerere Hogolo ambaye ni rafiki wa mwanafunzi huyo na Rino Mazoea, mkulima na mkazi wa Ikulu Hogolo wilayani Kongwa ambaye ni kaka wa marehemu.
Kamanda Zelothe Steven alisema wanamtafuta Aboubakar ambaye amekimbia kijijini hapo na hajulikani alipo mpaka sasa.
Katika tukio hilo, kaka wa marehemu ambaye pia anashikiliwa
Polisi, katika maelezo yake ya awali alidai kusikia purukushani zikitokea usiku wa tukio hilo la mauaji lakini hakutoka usiku huo
kushuhudia nini kinaendelea.
Mwanafunzi huyo alikuwa akiishi na babu na bibi yake kijijini hapo na siku ya tukio, walezi hao walikuwa wameondoka kwenda katika vijiji vya jirani, ambapo bibi yake alikuwa amekwenda Kongwa kwa ajili ya kujengea makaburi na babu yake alikwenda Kijiji cha Banyi Banyi kutembelea wagonjwa.
Naye Kareny Masasy kutoka Shinyanga anaripoti kuwa wanawake wawili (majina yamehifadhiwa) wamebakwa na watu watano waliovamia nyumba ya Nyerere Nalimi kwa mapanga na marungu na kujeruhi watu wengine watano sehemu mbalimbali za miili yao.
Watu hao wanadaiwa pia kupora fedha taslimu Sh milioni
17.7, simu mbili aina ya Nokia na begi moja la nguo mali ya majeruhi hao ambayo thamani yake haikufahamika.
Kamanda wa Polisi mkoani Shinyanga, Evarist Mangalla
alisema unyama huo ulifanyika katika Kitongoji cha Nyamhela Kijiji cha Mhongolo wilayani Kahama.
Kamanda aliwataja watu waliojeruhiwa kuwa ni Marco William (18), Idebuke Manyanda (31), Mayira Pili (75), Mateso Nyerere (26) na Nyerere Nalimi (53).
No comments:
Post a Comment