KUSHOTO: Shrien Dewani akiwa na mkewe, Anni. KULIA: Mziwamadoda Qwabe.
Muuaji wa kukodiwa amefichua madai mapya kwamba mauaji ya Anni Dewani wakati akiwa katika fungate ni agizo kutoka kwa mumewe.Mziwamadoda Qwabe alisema mauaji hayo ya mzaliwa wa Afrika Kusini yalipangwa kuonekana kama 'tukio la uhalifu'.
Alidai aliagizwa na mfanyabiashara Shrien Dewani 'aliyetaka mkewe auawe' na kwamba ionekane kama lilikuwa tukio la uporaji.
Qwabe mwenye miaka 27 alidai alisaidia kuteka nyara teksi ya wanandoa hao na alikuwa nyuma ya mpango huo pale muuaji wa pili aliposimama nyuma yake, kugeuka na kumpiga risasi Anni aliyekuwa na miaka 28, shingoni.
Stori iliyokuwa imefichika ya baba huyo wa watoto watatu ilianikwa hadharani kwenye maungamo yake yaliyosainiwa naye na kupokelewa katika Mahakama Kuu ya Cape Town, katikati ya wiki hii.
Alikiri kuteka, kupora, kumiliki bunduki bila kuwa na leseni na kisha kushiriki mauaji.
Wakati mashitaka haya kwa kawaida yanamfanya kukabiliwa na kifungo cha maisha jela, Qwabe alipokea miaka 25 na anastahili msamaha wa wafungwa katika miaka 17, chini ya vifungu vya ombi la uchunguzi dhidi ya Dewani mwenye miaka 32, anayeishi mjini Bristol.
Dewani kwa ukaidi alikataa tuhuma kwamba alipanga na kulipia mauaji hayo Novemba, 2010.
Katika usikilizwaji wa hivi karibuni kabisa wa kesi yake alieleza kwamba hayuko sawa kisaikolojia kuweza kurejea nchini Afrika Kusini kwa mashitaka kufuatia msongo mkubwa wa mawazo alionao.
Katika hati yake ya maungamo, Qwabe alimtaja Dewani kama mmoja wa washirika wake kwenye utekaji, uuaju na uporaji, na kusema alimpa kazi dereva teksi Zola Tongo, ambaye amehukumiwa kifungo cha miaka 18 kutokana na ushiriki wake kwenye mauaji hayo.
Katikati ya wiki hii, mjomba wa Anni, Ashok Hindocha alisema, "Tumefurahi. Watuhumiwa wawili wamepatikana na hatia. Sasa tunataka kujua nini hasa kilichotokea kwa Anni, kwanini walimuua."
Lakini akaongeza: "Ningekuwa na furaha mno kama watuhumiwa wote wangekuwa Afrika Kusini na uchunguzi ungefanyika na ukweli kuweza kujulikana.
"Kwetu, Anni bado hajafa. Hatujaanza taratibu za maombolezo. Hatuwezi. Tunahitaji kujua kilichotokea na kisha tunaweza kuanza kufanyia kazi suala hilo."

No comments:
Post a Comment