Tuesday, August 21, 2012

CHEKA TARATIBU...

Kinyozi mmoja kamnyoa nywele Mchungaji siku moja. Yule Mchungaji akajaribu kulipa lakini Kinyozi akakataa huku akisema, "Unafanya kazi ya Mungu." Asubuhi iliyofuata Kinyozi akakuta rundo la Biblia kwenye mlango wa saluni yake.
Siku nyingine Polisi akafika pale kunyolewa nywele, na kwa mara nyingine Kinyozi yule akakataa kupokea pesa ya Polisi yule huku akisema, "Unalinda jamii." Asubuhi iliyofuata Kinyozi akakuta rundo la Donati kwenye mlango wa saluni yake.
Siku nyingine tena Mwanasheria akafika kunyolewa, na kwa mara nyingine tena Kinyozi akakataa kupokea pesa huku akisema, "Unatumikia mfumo wa haki." Asubuhi iliyofuata Kinyozi akakuta msururu mrefu wa Wanasheria ukisubiri kunyolewa bure! Duh, balaa...

No comments: