Mume na mke wapo katika mazungumzo huku wakijiandaa kwenda kazini asubuhi. MUME: Kila mara unaweka picha yangu kwenye pochi yako na kwenda nayo kazini. Kwanini? MKE: Pale linapotokea tatizo, bila kujali ni kubwa kiasi gani, nikitazama tu picha yako tatizo linaondoka. MUME: Umeona nguvu na miujiza mikali niliyonayo? MKE: Ndiyo. Linapotokea huwa nashika picha yako na kujisemesha mwenyewe, "Kuna tatizo gani linaweza kuwa kubwa kuzidi hili?" Duh...

No comments:
Post a Comment