Thursday, August 16, 2012

CHEKA TARATIBU...

Wanandoa wawili wakiwa wamejipumzisha nyumbani ndipo mke akamwambia mumewe, "Nina habari njema kwako. Siku sio nyingi tutakuwa watatu hapa nyumbani badala ya wawili." Mume akamrukia mkewe na kumkumbatia huku akimbusu kwa fujo. Wakati akiendelea kumbusu, mke akaendelea kusema, "Nina furaha kwamba hali hiyo utaanza kuiona kesho asubuhi, mama yangu anakuja kuishi na sisi!" Ebo...

No comments: