Thursday, August 9, 2012

BINTI WA MIAKA 12 APOTEA KATIKA MAZINGIRA YA KUTATANISHA...

JUU: Polisi wakiendesha msako wa kumtafuta Tia. CHINI: Mama wa Tia, Natalie na rafiki yake wa kiume, David Niles. KULIA: Tia Sharp.
Wapelelezi wanajaribu kufuatilia mwenendo wa Tia Sharp masaa kadhaa kabla ya kupotea, kati ya taarifa za utatanishi kuhusu kama binti huyo mwanafunzi aliondoka nyumbani peke yake.
Wamepanga kumhoji mhusika wa dawa za kulevya Stuart Hazell, mtu wa mwisho kabisa ambaye anaaminika alimwona binti huyo mwenye miaka 12, kufuatia madai kwamba alimsindikiza hadi kwenye kituo cha treni ziendazo kasi.
Uamuzi huo umekuja baada ya mama wa Tia, Natalie mwenye miaka 30, kukiri: "Tunadhani ametoroshwa, lakini bado hatujui."
Familia ya Tia iliwaeleza polisi alitoroka nyumbani kwa bibi yake huko New Addington, South London, mchana wa Ijumaa kwenda kununua kandambili katika maduka ya Croydon's Whitgift yaliyoko umbali wa maili tano kutoka hapo.
Alikuwa nyumbani hapo na Hazell, ambaye ni rafiki wa kiume wa bibi yake kwa miaka mitano sasa, ambaye alitumikia kifungo jela kwa kumiliki panga na kujihusisha na dawa za kulevya aina ya cocaine.
Lakini juzi vita ya maneno ilifumuka ndani ya familia hiyo wakati ndugu wa Hazell mwenye miaka 37, ambaye ni mpaka rangi na mpambaji, kudai alimpeleka kwenye kituo cha treni.
Baba wa Hazell, Keith alisema: "Alinieleza alimsindikiza hadi kituo cha treni cha Addington ili kupanda treni kuelekea Croydon.
"Hakumwona akipanda treni lakini alimpeleka hadi kituoni hapo."
Dada wa Hazell, Sarah Parratt aliongeza: "Alikuwa mtu wa mwisho kumwona binti huyo na kushindwa kujua hasa kilichotokea.
"Alisema alikwenda naye karibu kabisa na mjini lakini kulikuwa na vurumai mno. "Alimpatia Pauni za Uingereza 11 za kununulia kandambili na kisha kumwacha hapo."
Lakini baba wa kambo wa Tia, David Niles mwenye miaka 29, alisisitiza Hazell alikuwa akifanya kazi za ndani kwenye nyumba ambayo walikuwa wakichangia na bibi wa binti huyo mwenye miaka 46, Christine, wakati alipotoweka.
Niles alisema: "Stuart alikuwa akifanya kazi za ndani wakati alipotoweka. Alikuwa akifuta vumbi, hakuweza kumsikia binti huyo.
"Baba yake…alimkosea. Stuart hakumpeleka binti huyo kituoni. Binti huyo aliondoka nyumbani peke yake."
Akiongeza utata kwenye jambo hilo, jirani amedai pia alimwona Tia akiondoka mwenyewe, ingawa muonekano wake haukuthibitishwa.
Polisi wameshindwa kupata picha zozote za CCTV ambazo zinaonesha Tia, mwanafunzi wa Raynes Park High School iliyoko mjini Merton, akiondoka eneo hilo.
Wapelelezi sasa wanataka kuongea na Hazell kupata uhakika wa lini hasa ilikuwa mara ya mwisho kumwona Tia. Mwaka 2003 alifungwa miaka miwili na miezi kumi jela kwa kusambaza cocaine baada ya kunaswa na polisi waliovaa kiraia. Mwaka 2010 alifungwa mwaka mmoja jela kwa kumiliki panga.
Natalie alisema bado ana matumaini ya kumpata licha ya shughuli ya kuwasha mishumaa usiku wa Jumatatu.
Alisema: "Tunaamini alichukuliwa lakini hatufahamu ni nani. Mtoto wa kike waliondoka na kutoweka."
Juzi Polisi walianzisha msako kwenye msitu umbali wa karibu maili moja kutoka nyumbani kwa bibi yake Tia.
Sharp aliungana na baba wa kambo wa Tia, David Niles mwenye miaka 29, ambaye alisema familia imeshikamana wakati msako wa binti huyo wa miaka 12 ukiingia katika siku ya nne na kuomba: "Endeleeni kumsaka binti yangu mdogo."

1 comment:

Anonymous said...

Appreciate the recommendation. Let me try it out.


my web page: diagnostic medical sonographer salary by state
Take a look at my homepage ultrasound programs