Thursday, August 9, 2012

CHEKA TARATIBU...

Jamaa mmoja alikuwa akiendesha gari kwenye mteremko mmoja ndipo simu yake ghafla ikaita. Alipoipokea akasikia sauti ya mke wake ikimuonya, "Mpenzi wangu, nimesikia redioni kuna mlevi mmoja anaendesha gari lake kwa fujo barabarani upande usio wake tena kwa spidi 200. Tafadhali kuwa makini sana!" Jamaa akajibu, "Sio gari moja mke wangu. Hapa sasa hivi napishana nayo kama mia moja!" Duh, balaa...

No comments: