Sunday, August 19, 2012

BAADA YA KUACHA UGAVANA, SCHWARZENEGGER SASA AJA NA "THE LAST STAND"...



Ni miaka kumi sasa tangu aanze kucheza filamu za mikikimikiki na kujikita kwenye ulimwengu wa watunisha misuli maarufu.Arnold Schwarzenegger sasa anajipanga kurejea kwenye skrini kubwa kupitia filamu yake ya kwanza kucheza tangu aache majukumu yake ya Ugavana wa California.Arnold mwenye miaka 65 aliitumia filamu ya The Expendables 2 kama sehemu ya kupiga jaramba kurejea kwenye fani kwa kuweka sawa vitu kadhaa katika filamu yake mpya ya The Last Stand.
Katika picha zake za kwanza za filamu hiyo iliyotumia bajeti kubwa zilizosambazwa hadharani watazamaji wanaweza kumwona Arnie akifanya vitu vyake bab-kubwa -akifyatua risasi kwenye bunduki yake kubwa na kuua vijana wakorofi.
Kwenye filamu hiyo anaonekana nyota huyo wa kwenye Terminator akikabiliana na changamoto kadhaa katika majukumu yake kama mkuu wa polisi wa mji mdogo unaoitwa Ray Owens ambaye analinda mji huo uliolala.
Baada ya kuondoka katika ofisi yake ya polisi akiwa kwenye nafasi ya kupambana na dawa za kulevya kufuatia kujihusisha na oparesheni iliyomwachia majuto katika kazi yake, Sheriff Owens akahama kabisa Los Angeles na kujikita katika maisha ya kupambana na uhalifu mdogo kila unapotokea katika mji wa mpakani wa
Sommerton Junction.
Baada ya kujituliza kwenye eneo lililo tulivu, mambo yakabadilika na utulivu uliokuwepo ukazimwa pale wafalme mashuhuri wa dawa za kulevya walipotoroka kwa namna ya kutisha kutoka gereza la msafara wa FBI.Kukiwa hakuna mwenye uwezo wa kuzuia, Arnie akawa mtu pekee aliyejitolea kupambana vilivyo na kuwaangamiza wafalme hao.
Schwarzenegger anaweza kuwa umri wake umekwenda kiasi fulani tangu alipotamba kwenye ulimwengu wa filamu, lakini nyota huyo wa Kindergarten Cop bado ni wazi ana uwezo wa kuwashika mashabiki wa filamu na kumimina risasi kwa staili ya kuvutia.
Filamu hii ya The Last Stand imepangwa kuzinduliwa mwaka 2013.

No comments: