Utoro wa wabunge bungeni, umeelezwa na wasomi na wanasiasa kuwa ni dalili mbaya kwa mhimili huo wa Dola na kuwa wameonesha bayana kutowajibika huku wakiwa mstari wa mbele kuwajibisha wengine.
Aidha, utoro huo unaelezwa kuonesha dhahiri kuwa wabunge wengi hawatambui thamani yao katika jengo hilo, huku wengine wakitaka watoro watangazwe hadharani.
Baada ya utoro huo wa wabunge kukemewa na Spika Anne Makinda kisha kusababisha Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika kukwama kupita, Spika ametakiwa kuwa makini kuhakikisha kunakuwa na mahudhurio yanayoridhisha kwa manufaa ya nchi.
Baadhi ya wasomi na wanasiasa walivitaka vyama vya siasa kuwajibika katika hilo, kwani inaonesha walisimamisha wagombea ubunge wasiofaa kuwakilisha wananchi.
Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala, Dk Benson Bana alisema utoro huo unatia wasiwasi uwajibikaji wa chombo hicho kwa wananchi.
Alisema utoro umetia doa kwa Bunge na kushauri kuundwa kwa chombo kitakacholidhibiti ambacho ni tume huru ya majaji ya kuangalia jinsi Bunge linavyotekeleza wajibu wake.
Alisema chombo hicho kitaangalia kanuni ambazo wanazitunga wao na kuzisimamia ikiwa ni pamoja na kudhibiti posho za wabunge hao.
Dk Bana alisema wabunge wameonesha wazi kuwa hawawezi kujidhibiti kwa kutumia kanuni, hivyo kupitia mjadala wa Katiba mpya kuwe na msisitizo wa kutoa maoni kwa chombo hicho huru ili kudhibiti wabunge.
Pia aliwataka wabunge warejee katika kuboresha kanuni zao na kuweka kanuni kuwa mbunge asipohudhuria bungeni bila ruhusa ya Spika kwa siku moja, asilipwe posho ya siku tatu huku mshahara wake pia ukikatwa.
"Bunge limedhihirisha haliwezi kujidhibiti kwa kujitungia kanuni na kuzivunja lenyewe, hivyo lazima wadhibitiwe kama wanavyodhibiti wengine, kwani Spika amekuwa laini na kuacha kanuni zinakanyagwa," alisisitiza.
Alitoa mfano wa Spika Makinda kukataza wabunge kutoka ovyo bila ruhusa yake au ya Waziri Mkuu, lakini wabunge wameendelea kutoka ovyo bila utaratibu.
Kiongozi wa Chadema, Profesa Mwesiga Baregu alisema utoro huo umeonesha wazi kuwa hawaelewi kipaumbele chao, kwani wabunge wanagombea nafasi hiyo na wala hawashinikizwi, hivyo watoro wameonesha kushindwa kazi.
Alisema hizo ni dalili mbaya katika uongozi, hivyo ni lazima kuangalia nidhamu ya vyama vya siasa kwani walipata ubunge kwa niaba ya vyama, hivyo hawana budi kuwajibika.
"Kwa jinsi hii inaonesha wazi kuwa vyama viliteua watu hao kugombea ubunge bila kuwa na sifa za kuwakilisha wananchi," alisisitiza.
Profesa Baregu alisema ni lazima Bunge na Spika wake wasimamie kanuni zao huku wakirejea katika kuziimarisha, ili kujenga nidhamu ikiwa ni pamoja na wananchi kupewa nafasi ya kuwawajibisha kabla ya miaka mitano.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Ananilea Nkya alisema utoro huo umeonesha dhahiri, kuwa kutowajibika huku kukiwa hakuna utawala bora kwa kutokuwapo nidhamu kwa wabunge.
Hivyo ni lazima kuhakikisha Spika anaweka utaratibu wa kutangaza wabunge wasiokuwapo bungeni kwa kila siku na walioko nje ya Bunge kwa sababu maalumu pia umma uelezwe.
Alisema hata kwa walio na dharura ziwekwe wazi, kwani wapo wanaoomba ruhusa na kwenda kwenye biashara zao, kisha mkutano wa Bunge unapomalizika watangazwe watoro ili kuwawajibisha kwa wananchi wao.
Alipinga kuundwa kwa chombo cha kuwajibisha wabunge kwa madai kwamba kitatumia fedha za wananchi huku akisisitiza, kuwa hata kuwakata posho na mishahara hakufai kwani kuna wabunge ambao hawana matatizo ya fedha na ndio wanatoroka kufanya biashara zao hivyo hawataumia.
Nkya alisema umma lazima uelezwe waliowatuma kuwawakilisha kuwa wapo au wana dharura gani, kwani kinachotakiwa kwa wabunge ni kufanya lile walilotumwa na wananchi.
Akizungumzia suala hilo, Katibu Mwenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema mbunge ni mwakilishi wa umma uliomchagua, kila mbunge ana wananchi waliompa dhamana ya kuwaongoza.
Alisema hivi karibuni kumekuwa na mahudhurio yasiyoridhisha kwa wabunge wengi katika vikao vya Bunge vinavyoendelea Dodoma.
"Hali hiyo haitoi picha nzuri, kwa wananchi waliowachagua ili wawasemee na kuwazungumzia kero zao, badala yake inawakatisha tamaa na kuwafanya wajisikie wanyonge na wasi na daraja la mawasiliano baina yao na Serikali," alisema
Alisema mwito wa CCM ni kwa kila mbunge kutekeleza wajibu wake, ili kesho na kesho kutwa, asijekuhukumiwa kwa jambo lisilo la msingi.
Alisema hata hivyo wabunge wa CCM wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha wanatimiza jukumu lao la kuwawakilisha wananchi wao na kuwasemea kero zao.
Aliasa kuwa jambo la msingi ni kuongeza juhudi katika kutekeleza hilo, ili wananchi waendelee kuwa na imani nao na chama chao.
Mbunge wa Kuteuliwa, James Mbatia ambaye ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi ambaye ndiye aliomba Mwongozo wa Spika na kuahirisha Bunge baada ya kugundua kuwa wabunge waliotaka kupitisha bajeti ya Wizara ya Kilimo hawafiki hata nusu, alisema wabunge hawajatambua thamani yao katika jengo hilo.
Alisema katika kanuni za Bunge hakuna kunapoonesha adhabu ya asiyehudhuria vikao katika mkutano mmoja, ila inaeleza kwa asiyehudhuria mikutano mitatu ya Bunge mfululizo bila taarifa, anakuwa amejifukuzisha Bunge.
Aliongeza kuwa katika Katiba ya nchi, ibara ya 94 inaeleza wazi kuwa ikiwa wabunge hawafiki nusu hawawezi kupitisha bajeti alisema kwa sasa Bunge lina wabunge 352 na nusu ni 176.
Alisema lakini kwa siku hiyo alihesabu mara ya kwanza walikuwa 98 na mara ya pili walikuwa 104 hivyo kusema 110 kwani alihisi wengine walikuwa nje.
Mbatia alisema hata wabunge waliokwenda Zanzibar kutokana na ajali ya meli wakijumlisha wa Zanzibar na wawakilishi hawazidi 60 na walioteuliwa na Bara kwenda Zanzibar ni 20 jumla wakawa 80.
"Sasa hawa wengine zaidi ya 96 wako wapi kwani Spika hawezi kutoa ruhusa kwa idadi kubwa hiyo ya wabunge kuwa nje ya Bunge," alisisitiza.
Alishauri kuwa ni vema wabunge wakaandaliwa semina ya kujitambua, kuwa wajibu wao kwanza ni kwa Taifa, jimbo, chama na mwisho maendeleo yao hivyo ni lazima kusimamia Serikali hususan wakati kama huu wa bajeti.
Alisema semina hiyo ya kujitambua itasaidia kupunguza malumbano bungeni kwa wabunge wote kuwa pamoja kwa maslahi ya Taifa.
"Wabunge hawajui thamani waliyobeba kwa Taifa, kwa nini wapo na wamefanya nini kwa Taifa lao, ni moja ya sababu za utoro bungeni," alisisitiza.
Spika mstaafu Pius Msekwa alionesha kuwatetea kuwa wakati mwingine wanakuwa na kazi zingine za Bunge nje ya jengo.
Pia alitanabahisha kuwa mahudhurio ya Bunge hutegemea jambo linalojadiliwa wakati huo, kwani haiwezekani wabunge wote wakawa bungeni wakati wote.
"Wakati Bunge linaendelea, pia kamati nyingine huendelea na shughuli zingine za Bunge hasa la bajeti ambalo hukaa kwa zaidi ya miezi miwili mfululizo, ni lazima wafikirie majukumu mengine," alisema
Msekwa alisema suala la wabunge kutokuwapo bila ruhusa ya Spika alitaka aachiwe Spika mwenyewe afanye kazi yake bila kuingiliwa, kwani ana mamlaka kamili.

No comments:
Post a Comment