Monday, July 23, 2012

HUKU 12 WAKIPOTEZA MAISHA, MAUZO YA FILAMU YA BATMAN YANATISHA...

Filamu ya "Dark Knight Rises" inazidi kupaa na sasa inaelekea kufikia mauzo ya Dola za Marekani milioni 160 kwa siku tatu za uzinduzi wake, licha ya balaa lililozingira siku ya uzinduzi, kwa mujibu wa ripoti.
Studio kubwa za Hollywood hazijatoa taarifa rasmi kuhusu mauzo mpaka sasa kwa kuheshimu wale wote walioathirika na shambulio la Ijumaa mjini Aurora...lakini taarifa zinakadiria filamu hiyo itafikisha mauzo ya Dola milioni 160.
Kabla ya shambulio la Ijumaa, filamu hiyo ilikadiriwa kuingiza takribani Dola milioni 170 kwa mujibu wa Jarida la The Hollywood Reporter.
Licha ya mahudhurio hafifu, filamu hiyo ya tatu katika mfululizo wa Batman za Christopher Nolan itamfanya kuvunja rekodi ya mauzo ya filamu yake ya "Dark Knight" aliyotoa mwaka jana ambayo iliingiza Dola milioni 158 katika wiki yake ya kwanza.
Filamu ya "The Avengers" bado inakamata usukani wa mauzo ya juu kabisa kuwahi kutokea katika uzinduzi ikiwa imefikisha Dola milioni 207.4.

No comments: