Habari zisizo rasmi zimedai kuwa mwigizaji maarufu wa Marekani Eddie Murphy amefariki muda mfupi baada ya kupata ajali akiwa kwenye michezo ya kuteleza kwenye theluji mapema leo.
Mwigizaji huyo na mwanafunzi wa kuteleza kwenye theluji alikuwa mapumzikoni katika klabu ya michezo hiyo ya Zermatt mjini Zermatt, Uswisi pamoja na familia yake na marafiki. Mashuhuda walieleza kwamba Eddie alishindwa kudhibiti ubao wake aliokanyagia na kujibamiza kwenye mti akiwa kwenye mwendo mkali.
Eddie Murphy alichukuliwa kwa ndege na timu ya doria ya mchezo huo hadi kwenye hopitali, licha ya kuaminika kwamba mwigizaji huyo alifariki palepale kutokana na kujibamiza huko.
Mwigizaji huyo alikuwa amevalia kofia ya kujikinga na ajali wakati wa ajali hiyo na kwamba dawa za kulevya na pombe havionekani kupewa nafasi kwamba vilichangia katika ajali hiyo.
Hii ni mara ya nne sasa kwa mwigizaji huyo kuripotiwa kufa kwa ajali kama hiyo.

No comments:
Post a Comment