Sunday, June 24, 2012

WAMACHINGA NJE YA MACHINGA COMPLEX...

Wafanyabiashara ndogondogo wa Dar es Salaam maarufu kama Wamachinga wakiendelea na biashara zao nje ya jengo maalumu kwa ajili ya wafanyabiashara hao la Machinga Complex lililoko Ilala, Dar es Salaam leo mchana. Wafanyabiashara hao wanalalamikia ushuru mkubwa unaotozwa na uongozi wa jengo hilo kuwa ni kikwazo kwa wao kufanyia biashara humo.

1 comment:

Anonymous said...

Serikali imefanya kosa kubwa sana kujenga mjengo huu wa machinga, Kitu kinachoharibu hapo katika mjengo ni kwamba wauzaji wapo katika vibanada vyao wengine juu wengine chini inakua biashara yao haionekani, na pia wanunuzi wanakua na uoga wa kuingia ndani ya mejngo haswa kwa wanwake hujui kitakachokutokea hupo wauzaji wengi ni wahuni na wavuta bangi kwa wewe na bahati yako, ni bora wangefanya maduka ya chini tu ya open kila mtu anaona na kuweza kujua anachotaka na hilo jengo likatwe kama vyumba au apartments na wasaidiwe wasiokua na uwezo au wasiokua na nyumba na sehemu za kuishi na kulala barabarabi.