Mwigizaji Kathryn Joosten, ama kwa wengi anafahamika kama Karen McKluskey katika tamthilia ya "Desperate Housewives" amefariki dunia juzi usiku baada ya kupambana kwa muda mrefu na maradhi ya kansa ya mapafu. Alikuwa na umri wa miaka 72.
Joosten ameshinda Tuzo za Emmy mwaka 2005 na 2008 kutokana na ushiriki wake wa kipekee kama Mwigizaji Mualikwa kwenye mfululizo wa filamu za vichekesho za "Housewives." Alichaguliwa kwa mara ya tatu mwaka 2010.
Joosten pia amecheza kama mke wa Landingham kwa misimu miwili katika shoo ya "The West Wing."
Aligundulika kwa mara ya kwanza kuwa ana kansa ya mapafu mwaka 2001 na ikamrudia Septemba 2009.
Mwakilishi wa mwigizaji huyo amesema alikuwa amezungukwa na familia yake wakati alipofariki.

No comments:
Post a Comment