Monday, June 25, 2012

MCHUMBA APIGWA STOP KUHUDHURIA MAZISHI YA RODNEY KING...

Mchumba wa Rodney King, Cynthia Kelley hakualikwa kwenye shughuli ya mazishi, familia ya King imeeleza.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, mazishi yatafanyika Jumamosi ijayo mjini Hollywood lakini familia haijawasiliana na Cynthia tangu baada ya kifo Rodney, na haijapanga kufanya hivyo.
Imeelezwa Cynthia hajashiriki chochote kwa ajili ya mipango ya mazishi ya Rodney, hivyo familia haioni umuhimu wa kumfuata.
Pia familia bado inashuku taarifa kuhusu Cynthia kwamba alimsikia Rodney akigonga dirisha majira ya saa 11 alfajiri siku ya Jumapili na kisha kusikia akianguka kwenye bwawa la kuogelea.
Familia haiamini kuwa Rodney alizama mwenyewe sababu kama ilivyobainishwa na chanzo kimoja cha habari, Rodney alikuwa muogeleaji mzuri sana.
Baadhi ya wanafamilia hawana kinyongo na Cynthia, lakini imeelezwa wengi wao hawataki kuzungumza naye tangu sababu rasmi za kifo chake kuwekwa hadharani.
Vyanzo vya kisheria zimesema, kifo cha Rodney bado kinachukuliwa kama ni ajali na hakuna dalili zozote za hujuma.

Juhudi za kumpata Cynthia hazikuzaa matunda.

No comments: