Sunday, June 24, 2012

KOCHA ATIWA HATIANI KWA KUBAKA WATOTO...

Kocha msaidizi wa zamani wa timu ya soka ya Penn State, Jerry Sandusky amekutwa na hatia ya udhalilishaji mtoto na hivyo kuwa hatarini kutumikia kifungo jela kwa maisha yake yote yaliyobaki.
Jerry amekutwa na hatia katika mashitaka 45 kati ya 48 yaliyohusisha wavulana 10 kwa kipindi cha zaidi ya miaka 15.
Baraza la mahakama lilifikia uamuzi huo baada ya kukaa kwa zaidi ya masaa 20. Jaji hakutaka kusubiri hadi Jumatatu hivyo alisoma hukumu majira ya saa 4 usiku.
Kocha huyo mwenye miaka 68 alionyesha kuguswa kidogo wakati hukumu ikisomwa mahakamani hapo.
Alipelekewa mara moja rumande, ambako atasubiria hukumu rasmi ambayo pengine itatolewa ndani ya kipindi cha miezi mitatu.
Waathirika 8 waliletwa mahakamani kumtambua Sandusky, na kuelezea jinsi kocha huyo wa zamani alivyowadhalilisha kwa kuwashikashika na kuwaamuru kuoga pamoja, kuwalazimisha kufanya ngono kawaida na kinyume cha maumbile.
Sandusky hakuruhusiwa kujitetea.
Mawakili wa Sandusky wameshutumu kwamba mashahidi hao wameshawishiwa kwa fedha, lakini utetezi uko sawasawa.
Sandusky amekutana na watoto wengi aliowadhalilisha kupitia Taasisi yake ya Second Mile ambayo alidai kuianzisha kwa ajili ya wavulana waliokosa fursa.
Mkurugenzi wa ufundi wa Penn State, Joe Paterno alifukuzwa kazi baada ya kashfa hiyo kwa kushindwakuchukua hatua za kutosha kufuatia ripoti ya 2001 kwamba Sandusky alimsumbua mtoto kwenye mabafu ya timu hiyo.
Hatahivyo, Paterno alifariki muda mfupi baadaye kutokana na maradhi ya saratani ya mapafu.

No comments: