Mrembo mwenye mvuto ameuawa kikatili na rafiki yake wa kiume wakiwa mapumzikoni huko Gran Canaria sababu alikuwa akiwasiliana na mpenzi wake wa zamani, polisi na waendesha mashitaka wanadai.
Sarah Shields mwenye miaka 23, alipigwa na kunyongwa hadi kufa naChris Chittock mwenye miaka 38, kabla ya kutupwa baharini akiwa uchi, imedaiwa na waendesha mashitaka wa kesi hii.
Familia yake ilitoa taarifa baada ya mrembo huyo kushindwa kurejea nyumbani kwao Ipswich, Suffolk, baada ya wiki mbili za mapumziko kwenye kisiwa kimoja Hispania.
Chittock anadaiwa kutuma meseji za simu kwa familia ya mpenzi wake huyo akidai amerejea Uingereza baada ya kuvunjika mahusiano yao.
Lakini mwili wake baadaye ulikokotwa na maji hadi ufukwe wa Balito, kituo maarufu cha watalii jirani na Puerto Rico kilichoko kusini-magharibi mwa Gran Canaria, nakuanzisha uchunguzi wa mauaji.
Chittock, ambaye aliishi na mpenzi wake huyo kijana, alikamatwa na kurejeshwa Hispania kufuatia mauaji hayo Julai 2010. Waendesha mashitaka wa Hispania wanataka afungwe miaka 20 jela kama akipatikana na hatia ya mauaji ya mpenzi wake.
Upande wa Mashitaka umedai kwamba Chittock alimshambulia Sarah baada ya kugundua kwamba amekuwa akiwasiliana na rafiki yake wa kiume wa zamani kupitia mtandao wa Facebook.
Mtuhumiwa, ambaye ni Mhandisi katika kampuni ya gesi ya BOC mjini Ipswich, alikutana na rafiki yake huyo wa kike kazini na wakaendelea pamoja kwa miezi minne kabla ya kwenye mapumzikoni.
Alituma kwenye Facebook akielezea furaha yake kwenda mapumzikoni na mpenzi wake kwa mara ya kwanza siku chache kabla ya kuachana.
Taarifa za kesi hii zimepatikana kwa mara ya kwanza kutoka kwenye hati ya upande wa mashitaka.
Imedaiwa kwamba Chittock alimpiga mpenzi wake huyo wakati wa ugomvi katika chumba chao kwenye Hoteli ya Balito Beach mjini Mogan.
Kisha Chittock akamkokota Sarah hadi ufukweni ambako alimkandika ngumi mara kadhaa usoni kabla ya kumnyonga, inadaiwa.
Uchunguzi umeonesha kwamba Sarah alivunjika pua.
Sarah inasemekana baadaye alivuliwa nguo zote, zikachomwa kwenye uwanja uliokuwa jirani kabla ya kuutosa mwili wake mtupu baharini.
Uchunguzi wa mwili wake umebaini kwamba Sarah alinyongwa.
Polisi wa Guardia aligundua mwili wa Sarah Julai 7, 2010, futi kama 50 kutoka baharini.
Mamlaka za Hispania zimepewa ruhusa ya kumshikilia Chittock rumande kwa miaka miwili wakati wakiandaa mashitaka.
Chittock alirejeshwa Hispania baada ya kupandishwa kizimbani mahakama ya South East Suffolk mjini Ipswich muda mfupi baada ya kurejea kutoka mapumzikoni.
Mahakama ilielezwa Julai 2010 jinsi Chittock alivyotuhumiwa kutuma meseji kutoka kwenye simu ya mpenzi wake.
Mwendesha mashitaka John Fenn alisema: "Chittock alirejea nchini kwake. Alirejea na simu ya mpenzi wake (Sarah).
"Katika maeneo mbalimbali, alituma meseji kutoka kwenye simu hiyo akijaribu kujenga picha kwamba Sarah yu hai na mzima, wakati ukweli ni kwamba aliuawa siku chache kabla."
Wakati wa kusikiliza shauri hilo, Wakali wa Utetezi Mark Holt alisema Chittock amekanusha kumuua Sarah.
Familia ya Sarah imeonesha wasiwasi wao kwamba waendesha mashitaka wa Hispania hawatawataarifu kesi hiyo ya mauaji itakapoanza.
Kaka mkubwa wa Sarah, Paul Davies amesema: "Inanilazimu kutafuta taarifa zozote mwenyewe. Tunaamini kesi itaanza Februari lakini hakuna yeyote aliyeweza kunithibitishia rasmi.
"Nimeongea na Wizara ya Mambo ya Nje na Ubalozi wa Uingereza lakini hakuna anayeonekana kuweza kuweka msukumo wa kesi, inaonekana mzaha kabisa.
"Tunahofia inaweza kuendelea bila sisi kujua.
"Mtu ataitaarifu familia ya Chittock, inaonekana sio haki kwamba hawalazimishi kutujulisha."

No comments:
Post a Comment