Kijana ambaye hakuweza kufahamika jina lake anayesadikiwa kuwa ni kibaka ameuawa na wananchi wenye hasira usiku wa kuamkia leo na kisha mwili wake kuchomwa moto hatua chache kutoka Kituo cha Polisi cha Chuo Kikuu, Dar es Salaam eneo la Mlimani.
Kwa mujibu wa walioshuhudia sakata hilo na baadhi ya askari waliofika eneo la tukio majira ya saa nne usiku, kijana huyo na wenzake kadhaa wanadaiwa kumvamia binti mmoja, mwanafunzi wa chuoni hapo kwenye barabara iendayo maeneo ya Changanyikeni na kutaka kumpora simu pamoja na fedha kabla ya binti huyo kupiga kelele za kuomba msaada na vibaka hao kutimka huku wakimwacha mwenzao mikononi mwa wananchi waliofika kutoa msaada.
Kijana huyo alipokea kipigo kitakatifu kutoka kwa wananchi hao na wanaoaminika kuwa wengi wao ni baadhi ya wanafunzi wa chuoni hapo ambao walielezea kuchoshwa kwao na vitendo vya wizi wa kutumia silaha unaoendeshwa na vibaka hao wanaotumia vizuri uwezo wa mapori kuzunguka chuo hicho. Polisi walifika eneo la tukio na baada ya taratibu kadhaa wakachukua mwili wa kijana huyo na kuondoka nao.

No comments:
Post a Comment