PICHANI: Rose enzi za uhai wake na kulia ni hospitali ambako alifia.
Kijana mmoja amekamatwa kuhusiana na kifo cha msichana mwenye miaka 15 kinachohisiwa kimetokana na dawa za kulevya.Rose Farley kutoka Liverpool, aliugua ghafla wakati wa sherehe ya siku ya kuzaliwa rafiki yake Ijumaa jioni na kufa alipofikishwa Hospitali ya Watoto ya Alder Hey Jumamosi asubuhi.
Wapelelezi wanachunguza tukio wakimshikilia kijana wa miaka 16 mkazi wa Liverpool juzi wakimtuhumu kuwa alipeleka dawa za kulevya katika sherehe hiyo.
Aliwekwa chini ya ulinzi kwa mahojiano ambako aliendelea kushikiliwa, Polisi wa Merseyside wamesema.
Kifo cha Rose kimekuja siku chache baada ya polisi kuonya vijana uwepo wa aina hatari za dawa za kulevya zinazozagaa katika eneo hilo.
Marafiki wa Rose wanahisi uwezekano wa mtu ama watu kudaiwa kuweka dawa hizo kwa siri katika kinywaji chake.
Rose alianguka baada ya kutumia jioni hiyo katika sherehe ya siku ya kuzaliwa rafiki yake kwenye klabu moja.
Msichana huyo alichukuliwa kwa gari la wagonjwa kutoka nyumbani kwake mjini Liverpool kwenda hospitali lakini akafariki muda mfupi baadaye majira ya saa 11 alfajiri.
Marafiki zake wamesema kwanza alianza kuumwa wakiwa kwenye klabu ya Silvestrian jirani na nyumbani kwake eneo la West Derby mjini humo.
Meseji mbalimbali zilitumwa kwenye mitandao ya kijamii na mtumiaji mmoja akiandika kwamba anatarajia waliohusika "watakamatwa".
Wazazi wa Rose, Chris na Lyn Farley walishatengana. Chris, mmiliki wa zamani wa klabu ya usiku, amewahi kwa nyakati tofauti kufanyakazi kama mlinzi wa Nahodha wa Liverpool na England, Steven Gerrard.
Mke mpya wa Chris, Kelly, ni rafiki mkubwa wa nahodha huyo, Alex, na wanandoa hao wamekuwa wakishirikiana mara kwa mara.
Kifo cha Rose kimekuja siku mbili baada ya Polisi wa Merseyside kutahadharisha uwepo wa dawa hatari za kulevya zilizo katika mfumo wa vidonge zilizosambazwa eneo la Kaskazini Magharibi.
Maofisa walishauri watu kutotumia vidonge hivyo vya rangi ya pinki, ambavyo vinajulikana mitaani kama 'Dr Death' au 'Pink McDonalds'. Onyo hilo limekuja baada ya vifo vya wanaume wawili ndani ya masaa 24 mjini Cambridgeshire wiki iliyopita. Mwanaume mmoja alikufa katika mazingira kama hayo mjini Bournemouth Mei 21.
Meseji za mwisho alizotuma Rose katika mtandao wa Intaneti zilionesha jinsi alipania kutoka usiku huo. Ijumaa, mwanafunzi alituma ujumbe katika mtandao wa Tweeter: "Oh, kifo kimetushangaza usiku wa leo."
Joyce Hale, meneja wa klabu hiyo alisema: "Kila kitu kilikuwa sawa usiku huo na hakukuwa na tatizo lolote. Tulikuja kujua baadaye nini kimetokea."
Maofisa walisema walikuwa na taarifa za kinywaji cha Rose kuwekwa dawa kwenye sherehe, lakini bado wanachukulia kifo chake kama kisichoelezeka.
Watu kadhaa wameweka meseji mbalimbali za maombolezo kwa msichana pamoja na maua katika lango kuu la shule ya North Liverpool Academy alikokuwa akisoma.

No comments:
Post a Comment