Maelfu ya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakiwa wamefurika kwenye Viwanja vya Jangwani katika mkutano mkubwa wa Kampeni ya kuchangia chama hicho inayojulikana kama "Movement For Change" juzi Jumamosi. Kufuatia kile walichodai viongozi wa Chadema kuwa viwanja hivyo vimekuwa vikikwepwa na vyama vingine, Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe akapendekeza viwanja hivyo viitwe rasmi "Chadema Square".
Mamia ya mashabiki na wanachama wa klabu ya Simba wakishiriki kwenye msafara wa timu hiyo katika Barabara ya Morogoro jana kusherehekea ubingwa wa Ligi Kuu ya Bara mwaka 2012 walioutwaa hivi karibuni na kumuenzi mchezaji wao, Patrick Mutesa Mafisango aliyefariki hivi karibuni kwa ajali ya gari maeneo ya Chang'ombe VETA, Dar es Salaam. Msafara huo uliishia Mbagala kwenye ukumbi wa Dar Live ambako kulifanyika sherehe kubwa.

No comments:
Post a Comment