Saturday, May 19, 2012

WILL SMITH AMNASA KIBAO ALIYEJARIBU KUMBUSU MDOMONI...


Mwimbaji na mcheza filamu maarufu, Will Smith mapema leo amemzaba kibao usoni mwandishi wa Ukraine wakati wa hafla ya kutambulisha filamu yake ya "Men in Black 4" mjini Moscow, Urusi.
Mwandishi huyo wa habari kutoka Ukraine alijaribu kumbusu Will mdomoni wakati nyota huyo akipita kwenye zulia jekundu ndipo Will akamsukuma kwa hasira na kisha kumnasa kibao.
Baada ya kumnasa kibao, Will alisema, "Ana bahati sana sikumshindilia ngumi."
Imefahamika baadaye kwamba jamaa huyo aliyembusu Will ni mwandishi wa kituo cha televisheni ambaye mara kwa mara amekuwa na tabia ya kuwabusu watu maarufu, yaani ni mtindo wake.
Kumbukumbu zinasema kwamba, Will amekuwa akiunga mkono ndoa za mashoga.

No comments: