KUSHOTO: Karla akiwa amepozi nje ya nyumba yake. JUU: Nyumba aliyokuwa akiishi Karla na wanawe watukutu. CHINI: Dirisha likiwa limefunikwa kwa ubao baada ya kioo kuvunjwa na watoto hao watukutu.
Mama mmoja aliyepachikwa jina la 'Ma Baker' baada ya kuwaachia wanawe watatu watukutu wafanye watakacho kwenye nyumba yao sasa ametimuliwa kabisa mjini.Karla Walker mwenye miaka 32, alifukuzwa kutoka kwenye nyumba aliyopanga mjin Prestwich, karibu na jiji la Manchester, baada ya kushindwa kuwadhibiti watoto wake ambao sasa wana umri wa miaka 11,12 na 13, na kusababisha kero kwa majirani zake kwa miaka mitatu.
Walivamia bustani, kurukia magari, kuangusha uzio na kuvunja madirisha.
Polisi katika malalamiko ambayo hayakutajwa ya lini wanadaiwa kufungulia muziki kwa sauti ya juu, sherehe za usiku wa manane na vijana hao kutukana ovyo.
Lakini Karla ambaye anafananishwa na Kate 'Ma' Baker ambaye alikuwa akiwatetea watoto wake wanne wahuni kwenye miaka ya 1930 nchini Marekani - amekumbana na maonyo mbalimbali ya kisheria kuhusu tabia za watoto wake hao.
Sasa amekuja juu kuhusu kutimuliwa kwake akisema watoto wake wamekuwa wakihusishwa na makosa yote maeneo ya jirani na kwamba anahitaji msaada mkubwa kutoka kwa mamlaka husika kuponya tabia za watoto hao.
Alifikishwa mahakama ya Manchester ambapo Jaji alimpa Karla mwezi mmoja kuhama kwenye nyumba hiyo Polefield kabla ya mwishoni kutimuliwa baada ya kushindwa kuondoka. Yeye na famila yake sasa wanaishi kwenye hosteli moja.
Lakini mmoja wa majirani mwenye miaka 53 ambaye ni dereva wa folk ambaye hakutaka kutajwa jina kwa hofu za kiusalama alisema tabia za watoto hao zimemgharimu kazi yake na hata kukaribia ndoa yake kuvunjika.
Alisema: "Nina amani sasa kwa familia hiyo kuondoka kwani walitufanya tuishi jehanamu kwa miaka sasa. Watoto wale walioshindikana walikuja kwenye bustani yangu, kukwea juu ya gari langu mara nyingi kiasi nashindwa kukumbuka ni mara ngapi nimemshitakia mama yao.
"Alipewa fursa kadhaa za kuhakikisha watoto wake wanarudi kwenye maadili lakini anaonekana kudhani halikuwa jukumu lake.
"Nashindwa kupata jibu na sidhani kama anaweza kuwadhibiti watoto wake. Nilimtaka kiungwana kuwaweka mbali watoto wake na mali zangu lakini aliweka maisha yangu matatani kwa kelele na lugha chafu na wakati wote yalitokea muda ambao walitakiwa kuwa shuleni.
"Hatukuweza kukaa kwenye bustani sababu ya lugha zao chafu. "Wanaweza kuporomosha matusi makubwa makubwa na kuniitia jina lolote baya.
"Mke wangu ni mwalimu hivyo walizoea kumdhihaki. Waliharibu gari na kumwingiza mbwa wao mchafu kwenye gari langu. Wanaye mbwa ambaye anaachiwa akirandaranda mitaani kwa majirani na ikafika wakati wakamuua. Jinsi gani aliwaruhusu watoto wake kutoka na mbwa huyo hata sifahamu.
"Iliniletea matatizo kwenye ndoa yangu na nikalazimika kuacha kazi sababu nilikuwa silali usiku na huku nikilazimika kuamka mapema kwenda kazini na nilikuwa nachoka sana. Nilimweleza meneja wangu kwamba sikuwa nahatarisha maisha yangu pekee bali hata ya watu wengine pia.
"Nilikuwa nikiathiriwa na mzio na ilikuwa kama nipo ndotoni. Nimekuwa nikiishi hapa kwa miaka takribani 25 na sikuwahi kuhama.
"Lakini utawezaje kuuza nyumba hali ukijua fika majirani zako watamweleza mnunuzi kila kitu kuhusu mahali hapo? Bado nimeathirika na mzio. Imeniathiri kisaikolojia. Hatimaye tutapata japo amani na utulivu."

No comments:
Post a Comment