KUSHOTO NA KULIA: Wazazi wa Shafilea, wakiingia mahakamani. KATIKATI: Shafilea (juu) na dada yake aliyeshuhudia mauaji (chini).
Binti mmoja ameuawa na wazazi wake wenye asili ya Pakistani kutokana na kile walichoamini kuiga maadili ya Ulaya kumeiletea aibu familia yao, mahakama imeelezwa juzi.
Miaka tisa baada ya binti yao Shafilea kufariki, Iftikhar na Farzana Ahmed wamepandishwa kizimbani wakituhumiwa kwa mauaji.
Mahakama imeelezwa kwamba polisi wamefungua kesi hiyo baada ya kuelezwa na dada wa marehemu kwamba aliwaona wazazi wake wakimuua Shafilea mwenye miaka 17.
Shafilea alikuwa akitaka kwenda chuo kikuu kusomea sheria na huko kulikuwa na marafiki wa kiume wanaowawinda wasichana wa rika lake, baraza la wazee wa mahakama limeelezwa.
Lakini wazazi wake wanadaiwa kuanzisha vurugu wakati wakijaribu kumlazimisha kufuata maadili asilia ya kimaisha ya kwao, kumrejesha Pakistan kwa ajili ya mipango ya harusi.
Huko Shafilea akanywa sumu na kulazimika kupandishwa ndege na kurejeshwa tena Uingereza kwa ajili ya matibabu. Alifariki akiwa nyumbani kwao Septemba, 2003 ikiwa ni siku chache baada ya kujiunga chuo na kuanza kazi za vibarua.
Wazazi wake walishindwa kutoa taarifa za kutoweka kwake, na ukimya huo ulivunjwa wiki moja baadaye na mwalimu wake. Mwili wake ulioharibika ulikutwa miezi mitano baadaye kwenye kando ya mto.
Mwendesha mashitaka, Andrew Edis alisema Shafilea 'alikuwa binti wa Kiingereza aliyevaa aina ya maisha ya Magharibi mwenye asili ya Pakistan' ambaye alitumbukia kwenye vurugu baada ya kupinga kukidhi matarajio ya wazazi wake.
"Watuhumiwa wakitumia zaidi ya miezi 12 kujaribu kubadili mawazo yake, walibaini kwamba hawawezi kufanikiwa na mwishowe wakamuua sababu maisha yake hayakukubalika katika familia hiyo na kuwaletea aibu kubwa," aliongeza.
Shafilea alikuwa mwanafunzi huko Warrington, Cheshire, ambaye alifurahia kufanya manunuzi kwenye maduka makubwa na kuvaa mavazi ya Kimagharibi, Mahakama ya Chester ilielezwa.
"Kwa hakika alitaka kuwa na marafiki wa kiume, kama ambavyo wasichana wa kati ya umri wa miaka 16 na 17 wafanyavyo," alisema Edis.
"Hicho ndicho kilichozusha msuguano, shinikizo na hasira katika familia hii. Wazazi wake walianza kuhitaji kumdhibiti."
Wakamnyang'anya simu yake ya mkononi ili kumzuia kuwapigia wavulana na alilalamika kwamba wazazi wake wamemuibia fedha kwenye akaunti yake ya benki.

Walimu na marafiki waliingilia kati pale alipokwenda shuleni akiwa na majeraha ambayo alisema yamesababishwa na wazazi wake, aliongeza Edis. Kisha Shafilea akaanza kuishi mbali na nyumbani kwao.

No comments:
Post a Comment