Bwana na Bibi Philpott wakiwa na watoto wao kabla ya tukio. KULIA: Wakiangua kilio wakati wa mkutano na waandishi wa habari baada ya kukamatwa jana.
Baba na mama wa watoto sita waliokufa baada ya nyumba yao kuteketea kwa moto wamekamatwa jana wakituhumiwa kwa mauaji ya watoto hao.
Katika mwendelezo wa aina yake, Mick Philpott mwenye miaka 55 na mkewe Mairead mwenye miaka 31 wanashikilia na polisi wakihojiwa na wapelelezi kuhusiana na tukio hilo la kutisha.Takribani wiki mbili zilizopita wanandoa hao, wote wenyeji wa Derby, walishindwa kujizuia na kumwaga machozi kwenye mkutano uliovuta hisia na waandishi wa habari huku wakati maofisa wa polisi wakielezea jinsi petroli ilivyomwagwa na kuwashwa moto.
Jade Philpott mwenye miaka 10 na wenzake John mwenye miaka 9, Jack mwenye miaka 7, Jessie mwenye miaka 6, na Jayden mwenye miaka mitano, wote walifariki dunia baada ya moto na moshi kuzuka kwenye nyumba yao ya Halmashauri ya Jiji huko Allenton, mjini Derby.
Kaka yao Duwayne mwenye miaka 13 alifariki akiwa hospitalini kutokana na majeraha siku chache baadaye huku wazazi wake wakiwa wamemzunguka kitandani.
Mkuu Msaidizi wa Polisi Konstebo Steve Cotterill alisema jana: "Nahisi kuna watu wamebaki na taarifa muhimu ambao bado hawajajitokeza kuongea nasi.
"Katika mtazamo wa kukamatwa, ningeshauri ambao wamenyamaza na taarifa, wakiwa hawapendi kusikika maoni yao hadharani au hawajiamini, wafanye hivyo sasa.
"Binafsi nawahakikishia kwamba tutazifanyia kazi taarifa zao kwa umakini mkubwa.
"Bado tunahitaji taarifa za kutusaidia katika tukio hili.
"Kukamatwa hawa wa mwanzo ni hatua moja tu mbele katika uchunguzi.
"Ni muhimu sana kama unajua chochote kinachoweza kutusaidia, jitokeze sasa, usiendelee kusubiri tena.
"Ni muhimu kwamba tunatafuta haki ya hawa watoto sita."
Cotterill amefafanua kwamba uchunguzi bado unaendelea na kwamba ni mlolongo mrefu sana.
Aliongeza: "Japokuwa moto ulitokea zaidi ya wiki mbili zilizopita, hili ni tukio lenye utata na itatuchukua muda mrefu kuliunganisha pamoja tukio hili kuanzia jioni ya janga lenyewe.
"Nafahamu kesi hii imeigusa mno jamii na wakazi wanahitaji majibu jinsi lilivyotokea na kwa sababu gani.
"Lakini ningewataka wawe watulivu na kuendelea kuonesha ushirikiano waliotupa mpaka sasa. Uchunguzi wetu ni wa kina na kuumiza na itawachukua muda mrefu."
Wiki moja iliyopita, polisi waliondoa basi dogo na trela lake linalodhaniwa lilikuwa likitumiwa kama makazi ya ziada kwa familia hiyo, huku bwana na bibi Philpott mara moja moja wakilala humo nje ya nyumba.

No comments:
Post a Comment