KUSHOTO: Mtakatifu Barnabas. JUU: Jumba ambamo waraka huo unahifadhiwa kwa sasa. CHINI: Waraka wenyewe ulioandikwa kwenye kipande cha ngozi ya mnyama ambao unakisiwa kuandikwa katika karne ya tano.
Waraka uliomo katika kipande cha ngozi, ukiaminika uliandikwa karne ya tano lakini ukagundulika miaka 12 tu iliyopita, utasababisha kuanguka kwa Ukristo duniani, inadai hivyo Iran.Waraka, ulioandikwa kwenye ngozi ya mnyama, kwa kifupi unaelezea jinsi Yesu alivyotanabaisha na yeye mwenyewe kutabiri ujio wa Mtume Muhammad, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Iran.
Ukiwa umeandikwa kwa lugha ya Syria, umedai injili pia imetabiri ujio wa Masia wa mwisho wa Kiislamu, ripoti zimeongeza.
Mamlaka za Uturuki zinaamini inawezekana kuwa ni chapisho la Injili ambalo Yesu alimpatia Barnabas, ripoti za vyombo vya habari vya Iran zimedai kwamba waraka huo utachangia kuanguka kwa Ukristo kwa kudhihirisha Uislamu ni dini sahihi.
Gazeti la Basij linadai katika Sura ya 41 ya Injili inasomeka: "Mungu alijificha wakati Malaika Michael akiwatimua Adam na Eva kutoka peponi, na Adam alipogeuka, akaona juu ya lango la peponi pameandikwa "La elah ela Allah, Mohamad rasool Allah" ikimaanisha, "Allah ndiye Mungu pekee na Muhammad ni Mtume wake."
Mamlaka za Uturuki zimeupiga marufuku waraka huo mwaka 2000 uliokuwa ukimilikiwa na genge la wahuni walioshitakiwa kwa makosa ya uhalifu na kumiliki mabomu.
Lakini mshangao wa kugundulika waraka huo umeshamiri zaidi Februari mwaka huu pale iliporipotiwa kwamba Vatican wametuma maombi rasmi ya kupatiwa waraka huo. Haijafahamika kama ombi hilo limekubaliwa au la.
Asili yake haijafahamika, lakini gazeti la National Turk limeripoti kwamba waraka huo umehifadhiwa katika ofisi za Justice Palace lililoko mji mkuu wa nchi hiyo, Ankara, na kwamba utahamishwa chini ya ulinzi mkali wa polisi kutelekwa Jumba la Makumbusho la Nyaraka za Kale mjini humo.
Gazeti la Basij linashauri kwamba uvumbuzi huo ni nyeti mno kwamba unaweza kutikisa siasa za dunia.
"Uvumbuzi wa Biblia halisi ya Barnabas sasa unaweza kushusha thamani ya Kanisa la Kikristo na mamlaka zake na unaweza kuleta mapinduzi ya kidini duniani," limeeleza.
"Ukweli ni kwamba, Biblia hii imetabiri ujio wa Mtume Muhammad na wenyewe ndani umebainisha dini ya Kiislamu."
Hata hivyo, Mamlaka za Uturuki zinaamini waraka huo haujachakachuliwa, huku wachunguzi wengine wa mambo wamehoji aina yake ya uandishi uliotumika.
Erick Stakelbeck, mchambuzi wa ugaidi na mchunguzi wa karibu wa mambo ya Iran, alisema: "Mkakati wa Wairani umelenga kutokomeza Ukristo kwa ghara yoyote, ikibidi kupotosha maandiko, kuchoma Biblia au kushambulia makanisa yanayochipukia."

No comments:
Post a Comment