Friday, May 18, 2012

WABAMBWA WAKIFANYA NGONO KWENYE TEKSI...

JUU: Michelle Palmer (kushoto) na Vince Acors. CHINI: Mandhari ya Dubai ambako sheria kali za Kiislamu zinatumika. KULIA: Rebecca Blake.

Mwanamke mfanyabiashara wa Uingereza anakabiliwa na kifungo cha miaka mitatu jela kwa tuhuma za kufanya ngono ndani ya teksi mjini Dubai akiwa amelewa.
Rebecca Blake mwenye miaka 29 na Conor McRedmond walikamatwa baada ya kuchapa kilevi kutwa nzima.
Walishikiliwa kwa siku tano na kutuhumiwa kufanya ngono nje ya ndoa na kulewa hadharani, yote yakiwa ni makosa ya jinai kwa mujibu wa sheria kali za Kiislamu nchini humo.
Rebecca, mshauri wa masuala ya ajira, alikutana na Conor ambaye ni raia wa Ireland kwenye hoteli ya Irish Village ambako kila mtu huchajiwa Pauni 10 za Uingereza ikiwa ni ada ya kunywa siku nzima. Baada ya kunywa kwa masaa 12, wawili hao walikodi teksi kuelekea Dubai Marina.
Dakika kadhaa baadaye walinaswa na dereva wa teksi hiyo kupitia vioo wakiwa kwenye mahaba mazito, kwa mujibu wa ripoti za polisi.
Kufuatia kukerwa na tabia zao, dereva huyo aliamua kusimamisha gari na kwenda kulalamika kwa polisi wa doria aliyekuwa ameegesha gari lake jirani. Aliporejea akiwa na polisi, walimuona Rebecca akifanya ngono kwenye kiti cha nyuma cha gari na Conor, imedaiwa.
Chanzo cha habari kimesema: "Walikuwa wamelewa sana, wakaanza kubusiana na kisha kuanza uchafu wao. Hapo ndipo wakaanza ngono.
"Wakati polisi alipokwenda pale, alikuta mwanamke akiwa mtupu kabisa na wakifanya ngono katika kiti cha nyuma cha teksi hiyo."
Rebecca anafanya kazi kwenye taasisi kubwa ya kutafutia watu ajira ya Manpower mjini Dubai. Anatokea Croydon, mashariki mwa London na alipata elimu yake kwenye Shule ya Sekondari ya Kanisa Katoliki.
Baada ya kukamatwa kwao, wawili hao walipelekwa kituo jirani cha polisi cha Jebel Ali na kuwekwa rumande tangu Mei 4 hadi Mei 9. Polisi walichukua kipimo cha DNA kama uthibitisho kwamba walifanya ngono na kwamba walikuwa wamelewa.
Maofisa wanangojea majibu ya vipimo hivyo kutoka maabara kabla ya kuwafikisha mahakamani. Waliachiwa kwa dhamana kutoka kwa watu wawili tofauti ambao ni marafiki zao ambao walikabidhi pasi zao za kusafiria.
Rebecca alidhaminiwa na meneja wa kampuni hiyo, Rowley Rees Brown mwenye miaka 42, rafiki yake anayeishi Dubai.
Jana, Rebecca alikanusha kukamatwa kwa kufanya ngono na kusisitiza kuwa alikuwa peke yake kwenye kiti cha nyuma cha teksi hiyo. Katika mahojiano, aliripotiwa kusema kwamba: "Sifahamu madai hayo ya kufanya ngono yanatokea wapi. Nimekamatwa kwa kukutwa na chupa ya bia ndani ya teksi, si kufanya ngono. Ni hivyo tu. Nilikuwa peke yangu kwenye gari."
Conor, ambaye anadhaniwa kufanya kazi ya uhandisi kwenye kampuni moja, naye amekana mashitaka.
Yeyote anayekutwa na hatia ya kutembea nje ya ndoa anakabiliwa na kifungo cha kati ya mwezi mmoja na miaka mitatu kwa mujibu wa sheria za Dubai.
Hukumu kwa matumizi ya vilevi ni hadi miezi sita jela na faini inayofikia Pauni 340 za Uingereza.
Wageni wanaohukumiwa Dubai hurejeshwa makwao mara wamalizapo vivungo vyao.
Kesi hiyo inaonesha ugumu wanaokabiliana nao zaidi ya Waingereza 100,000 wanaoishi Dubai. Maofisa wa serikali ya Ghuba wamewashitaki Waingereza kadhaa kutokana na vitendo mbalimbali vya uvunjaji sheria katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.
Mwaka 2008, Vince Acors wa Bromley, mjini Kent na Michelle Palmer wa Oakham, Rutland walihukumiwa kifungo cha miezi mitatu jela baada ya kukutwa wakifanya ngono kwenye ufukwe wa Jumeirah. Wanadaiwa kukutwa wakibusiana na kukumbatiana na hukumu yao ilisitishwa kwa muda kutokana na pingamizi lililowekwa.

No comments: